Mbwana Samatta akishangilia moja ya goli aliloifungia Taifa Stars mechi za nyuma
Na Baraka
Mpenja, Dar es salaam
Imechapishwa Julai 18, 2014, saa 9:00 asubuhi
TAIFA
Stars chini ya kocha, Mholanzi, Mart Nooij, inakabiliwa na mechi muhimu dhidi
ya Msumbiji `Black Mambas` , kuwania kupangwa hatua ya makundi kusaka tiketi ya
kwenda kushiriki fainali za mataifa ya Afrika, AFCON , mwakani nchini Morocco.
Mechi hiyo
ya kwanza itapigwa jumapili (julai 20 mwaka huu) ndani ya uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam , ambapo Stars
watalazimika kupata ushindi wa mabao
angalau 3-0 ili kujiweka mazingira mazuri ya kusonga mbele katika mechi ya
marudiano itakayochezwa wiki mbili baadaye mjini Maputo nchini Msumbiji.
Kuelekea
katika mechi hiyo ya jumapili, unaweza kusema kikosi cha Taifa Stars kipo
kamili gado kwasababu nyota wake wote wa ndani na nje wapo tayari kwa kazi.
Mwinyi
Kazimoto Mwitula alitua jana asubuhi akitokea nchini Qatar anakocheza soka la kulipwa
tayari kwa kuongeza nguvu katika kikosi cha Stars.
Uzoefu wa
Mwinyi katika soka la kimataifa utasaidia sana kuimarisha safu ya kiungo
itakayomkosa Frank Domayo `Chumvi`
kwasababu ni majeruhi.
`Majembe`
mawili ya Stars yanayokipiga TP Mazembe ya DR Congo, Mbwana Ally Samatta na
Thomas Ulimwengu yapo nchini tangu juzi.
Kuelekea katika
mechi hiyo, Mart Nooij ana wigo mpana wa kuamua nani aanze katika safu ya ushambuliaji.
Samatta amesema
kwa upande wake, maandalizi ya mechi hiyo yamekamilika na amefurahi kwasababu
ni mzima wa afya tofauti ni ilivyokuwa kwa mechi iliyopita mjini Harare nchini
Zimbabwe.
“Maandilizi
kwa mimi kama mimi yako vizuri , kwasababu
tulikuwa katika maandalizi ya ligi ya mabingwa, tulikuwa tunafanya mazoezi
magumu. Kwahiyo maandalizi yako vizuri kwangu na kwa Thomas pia”. Alisema Samatta.
Thomas Emmanuel Ulimwengu
Ulimwengu
kwa upande wake, kauli aliyoitoa jana jioni ni kwamba mechi ya jumapili itakuwa
ngumu, lakini watajitahidi kupambana ili kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.
“Maandilizi
ni mazuri, tumefanya mazoezi, tunaamini tutafanya kazi nzuri. Mechi itakuwa
ngumu, lakini tutafanikiwa kwa umoja”.
“Tutafanya
kazi, tuwaombe watanzania waje kwa wingi uwanjani, ushindi wa pili ni kwa
upande wao”. Alisema Ulimwengu.
Mshindi
wa jumla kati ya Tanzania na Msumbiji atakata tiketi ya kupangwa katika hatua
ya mwisho ya makundu kutafuta safari ya Morocco.
Tanzania
iliitoa Zimbabwe kwa kuifunga bao 1-0 uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na
kulazimisha sare ya mabao 2-2 mjini Harare.
Msumbiji
wao waliifunga Sudan Kusini mabao 5-0 mjini Maputo na walipoenda ugenini
walilazimisha suluhu ya bila kufungana.
Kila la
kheri timu ya taifa ya Tanzania, Taifa stars kuelekea mechi muhimu na `Black
Mambas`.
0 comments:
Post a Comment