Imechapishwa Julai 31, 2014, saa 9:23 alasiri
NEYMAR ameweka wazi kuwa atarudi uwanjani agosti 18
mwaka huu kuitumikia Barcelona katika mechi ya maandalizi ya kabla ya msimu ya
kombe la Joan Gamper dhidi ya Leon.
Mbrazil huyo alivunjika mfupa wa uti wa mgongo
wakati wa mechi ya robo fainali ya kombe la dunia dhidi ya Colombia na
alizikosa mechi mbili.
Neymar aliwakosa Ujerumani, hatua ya nusu fainali
na Uholanzi mechi ya mshindi wa tatu.
Hata hivyo anatarajia kujiunga na Barcelona katika
maandalizi ya msimu Agosti 5 mwaka huu na ataweza kucheza kwenye mechi ya
Gamper ndani ya dimba la Camp Nou.
“Naimarika taratibu kutokana na majeruhi. Nitarudi
Barcelona kwa asilimia 100,” aliwaambia waandishi wa habari nchini Brazil.
“Nahitaji kuwa na msimu mzuri na naangalia mbele
kuwasaidia wachezaji wenzangu kupata matokeo mazuri. Pia nahitaji kuisaidia
timu ya Brazil.
“Nina imani ya kucheza mechi ya Gamper Agosti 18.”
0 comments:
Post a Comment