Van Gaal alikuwa na tabasamu kubwa wakati wa mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari katika klabu ya Manchester United manager.
Imechapishwa Julai 18, 2014, saa 11:57 jioni
LOUIS van Gaal hataleta kombe la ligi kuu Manchester United katika msimu wake kwa kwanza, kwa mujibu wa kocha wa Queens Park Rangers, Harry Redknapp.
Redknapp, aliyekamilisha usajili wa beki wa zamani wa United, Rio Ferdinand jana alhamisi, haoni kama Mholanzi huyo atapata kombe bila kuwa na wachezaji wanne wa kiwango cha juu, achalia mbali Luke Shaw na Ander Herrera waliosajiliwa.
'Van Gaal ana rekodi nzuri, lakini wanahitaji wachezaji," .Redknapp aliwaambia talkSPORT.
Bosi mpya wa United alipata nafasi ya kujua mazingira ya klabu akiwa na gwiji wa klabu hiyo Sir Bobby Charlton.
"Anahitaji kuleta wachezaji angalau wanne au watano ili kurudi pale alipokuwa Alex (Ferguson), ambapo walishinda makombe".
"Kwa hatua hii kama ingekuwa ni kucheza kamari ya wao kushinda ubingwa msimu ujao, nisingewapa nafasi ya kushinda, vinginevyo wanasajili wachezaji watatu au wanne wa kiwango cha juu".
Redknapp alitaja washindani wa ubingwa msimu ujao kuwa ni Chelsea, Manchester City na Arsenal na kusema Man United watahangaika kufika juu baada ya kushuka wakati wa David Moyes.
Kocha wa QPR alizungumza na waandishi wa habari leo asubuhi.
Jembe jipya: Rio Ferdinand (kushoto) akishiriki mazoezi yake kwa mara ya kwanza leo asubuhi katika klabu ya QPR
"Sioni kama watakuwa imara kama Chelsea au Man City," aliongeza. "Nadhani Asernal wamefanya usajili mkubwa kwa kumleta Alexis Sanchez, kwahiyo msimu ujao wanaweza kuukaribia ubingwa zaidi".
"Bado ni wazi. Ningependa kuwaona Liverpool wanakuwa na msimu mzuri tena, lakini wamempoteza mchezaji wa ajabu (Luis Suarez). Hana mbadala kwakweli".
Alexis Sanchez amesajiliwa na Asernal kutokea klabu ya Barcelona
0 comments:
Post a Comment