Thursday, July 31, 2014

Retirement is not a possibility - Ronaldinho
Imechapishwa Julai 31, 2014, saa 5:14 asubuhi

GWIJI wa Brazil, Ronaldinho ‘Gaucho’ amethibitisha kuwa ataondoka Atletico Mineiro, lakini hayupo tayari kustaafu soka.

Nyota huyo mwenye miaka 34 alifurahia maisha yake ya soka kwa kufanya makubwa akiwa na klabu za Paris Saint-Germain, Barcelona na AC Milan.

Alishinda mechi 99 na kubeba kombe la dunia mwaka 2002 akiwa na timu ya taifa ya Brazil nchini Japan na Korea kusini.

Tangu aondoke San Siro mwaka 2010, mchezaji huyo mzaliwa wa Porto Alegre alirudi nchini BrazIl, akijiunga na timu ya Flamengo na baadaye Atletico ambapo alishinda kombe la Copa Libertadores na sasa anaamini bado anahitaji kucheza soka zaidi.

“Kustaafu kwasasa,  haiwezekani,” aliviambia vyombo vya habari.


“Kwa muda huu kaka yangu( wakala Roberto de Assis) anafikiria kila kitu. Kuanzia wiki ijayo, tutazungumzia hatima yangu ya baadaye. Nitatumia siku hizi chache kukaa mbali na mambo yote ya soka na kupumzika. Lakini najua simu yake inapigwa sana”.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video