Imechapishwa Julai 24, 2014, saa 2:52 usiku
BOSI wa Bayern Munich, Pep Guardiol amesema
walijitahidi kufanya kila kitu kumshawishi Toni Kroos asaini mkataba mpya
Allianz Arena.
Nyota huyo mwenye miaka 24 alijiunga na Real
Madrid mwezi huu baada ya mazungumzo na Bayern juu ya mkataba mpya kuvunjika
mapema mwaka huu.
Guardiola alikiri kuwa mabingwa hao wa Bundesliga
walimshawishi mshindi huyo wa kombe la dunia kuendelea kubakia klabuni na
kushindikana, lakini Bayern imemtakia maisha mema katika maisha yake mapya ya
soka.
“Tulijitajiihi kumshawishi abakie klabuni, lakini
naelewa. Ni kijana na anataka changamoto mpya. Ni maamuzi yake na
tumeyaheshimu,” aliwaambia waandishi wa habari.
“Natumaini ana furaha Madrid. Ilikuwa heshima kuwa
kocha wake. Namtakia kila la kheri yeye na familia yake. Wakati huo huo napenda
kumshukuru kwa yale aliyofanya msimu uliopita”.
0 comments:
Post a Comment