Makamu wa Rais wa Simba sc, Geofrey Nyange `Kaburu` amepania kuendeleza soka la vijana klabu hapo.
Na Baraka
Mpenja, Dar es salaam
0712461976
Imechapishwa Julai 13, 2014, saa 10:24 jioni
MAKAMU wa Rais
wa Simba sc, Geofrey Nyange `Kaburu` ni miongoni mwa watu wenye mtazamo sahihi
katika soka la vijana nchini Tanzania.
Inawezekana
ana mapungufu yake kama ilivyo kwa mtu yeyote, lakini mara zote mtazamo wake wa
kuendeleza soka la vijana katika klabu ya Simba unanivutia sana.
Ili
kutengeneza mfumo na falsafa ya klabu, huwezi kukwepa soka la vijana. Timu kama
Barcelona zilianzisha mpira wa aina ya `Tiki -taka` . Huu ni mfumo wa kucheza
mpira kwa kumiliki maeneo yote muhimu ya uwanja.
Mpira huu huwa
wachezaji hawasimami eneo moja kama ilivyo kwa mifumo mingine. Wachezaji
wanatakiwa kubadilishana nafasi kadri wawezavyo. Mlinda mlango pekee ndiye
mchezaji anayebaki eneo moja.
Katika mfumo
wa `Tiki-Taka`, beki anaweza kuwa mshambuliaji, kiungo anaweza kuwa beki,
mshambuliaji anaweza kuwa beki ndani ya uwanja. Yaani kama beki wa kati
amepanda, kiungo wa kati anarudi kukaba nafasi yake. Kama beki wa kulia
amepanda kupandisha mashambulizi, winga wa kulia anaweza kushuka katika nafasi
ya kulia kuzuia.
Ninachojaribu
kusema ni kwamba kwenye mpira wa `Tiki-taka`, hakuna kukaa nafasi moja, yaani
kama ni namba tisa unaweza kuwa mlinzi kwa muda wowote uwanjani au beki unaweza
kushambulia .
Ramadhan Singano `Messi` (kulia) ni zao la Simba B
Huu ndio mpira
waliocheza Barcelona kwa muda mrefu tangu wauasisi mwaka 1990, Mlanzi Johan Cruyff
akiwemo. Walifanikiwa kuzisumbua timu nyingi za dunia hii. Haikuwa rahisi
kuifunga Barca, na kwakuwa wachezaji wengi wa Barcelona walikuwa wanacheza timu
ya taifa, wakajikuta wanahamishiwa mfumo huo kwa soka zima la Hispania.
Siku za
karibuni, `Tiki-taka football` imekumbana na changamoto. Watu wamejua namba ya
kucheza na mfumo huu. Hii inawalazimu Barca na Hispania kukaa chini kuboresha
zaidi mpira huu na kuleta mpango B kwasabau huu unaelekeka kushindwa. Si kwamba
mpira huu umekwisha, lakini wanatakiwa kuufanyia maboresho.
Ili ufanikiwe
kucheza `Tiki-taka football`, moja ya vitu vya kuzingatia ni kuwa na wachezaji
ambao wanaweza kucheza nafasi tofauti tofauti uwanjani.
Kwa maana ya
mchezaji awe na uwezo wa kusimama nafasi tofauti, ili pale anapotakiwa kuwa
beki anatakiwa kufanya hivyo. Na ili kuwapata wachezaji wa aina hii, lazima uwe
na akademi za vijana wenye umri tofauti.
Barcelona wana
akademi za vijana wa kila aina, wapo 6-10, 10-12, 12-14, 14-16, 16-17, 17-18,
na kadhalika. Kwa mfumo huu ni rahisi kumuendeleza mchezaji na kumfundisha
nafasi tofauti tofauti uwanjani.
Harun Chanongo (kulia) akiwakimbizi mabeki wa FC Libolo ya Angola kwenye moja ya mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika. Nyota huyo ni zao la Simba B
Tiki-taka ni
mfumo unaohitaji muda mrefu sana kufikia malengo.
Kaburu wa
Simba wakati akiwa makamu mwenyekiti wa klabu hiyo enzi za utawala wa Ismail
Aden Rage, alifanya kazi kubwa kuhakikisha Simba ya vijana maarufu kama Simba B
inakuwa na mafanikio.
Kocha msaidizi
wa Simba, Suleiman Abdallah Matola `Veron`, na aliyekuwa mjumbe wa kamati ya
utendaji ya Simba, Ibrahim Masoud `Maestro` wakisaidiana na Kaburu walifanikiwa
kuzalisha vijana wazuri.
Ramadhan
Singano `Messi`, Said Ndemla, Jonas Mkude, Harun Chanongo, Edward Christopher,
Wiliam Lucian `Gallas` ni moja ya matunda ya mpango huu makini.
Simba na Azam
zimekuwa klabu za mfano kwa soka la vijana. Wengine wanajikongoja, lakini kwa
klabu hizi mbili angalau zina mwelekeo ingawa kuna changamoto.
Siku chache
zilizopita, Kaburu alisimamia usajili wa wachezaji wawili vijana chini ya miaka
20, Peter Manyika Junior pamoja na beki kinda wa Mwadui ya Shinyanga, Ibrahim
Hajibu Migomba.
Jonas Mkude ni tunda la Simba B
Baada ya
usajili huo, Kaburu alisema malengo ni kuijengga Simba B.
Kwa hili
nampongeza Kaburu na wenzake, lakini nadhani imefika wakati wa Simba kuwa na
mfumo rasmi wa kupata wachezaji wake.
Kama wanataka
kuifanya Simba kuwa klabu bora, lazima viongozi wajikunje kujenga akademi ya soka la vijana. Lengo liwe ni kuchukua
vijana wa umri mdogo zaidi na kukuzwa katika mfumo na utamaduni wa Simba.
Hii itaifanya
kuwa klabu ya kisasa. Kwanza wachezaji watakaozalishwa watakuwa wazalendo kwa
Simba. Kama mchezaji amekulia katika mazingira ya Simba, lazima aipende klabu
yake.
Uliona
Fabregas, alikuwa Asernal, lakini bado akili ilikuwa Barcelona. Leo hii huwezi
kumuondoa, Lionel Messi, Iniesta, Harnandez
katika klabu ya Barcelona. Wamekaa kwa muda mrefu na wanaona utumwa kutoka
Katalunya.
Ili kuiga
hili, Kaburu lazima awekeze muda na
fedha katika soka la vijana. Inaweza kuwa ngumu kutokana na uwezo wa klabu,
lakini naamini Simba ina uwezo wa kufanya hivyo kama nia itakuwepo.
Amini
usiamini, mpango huu wa soka la vijana utaibadilisha Simba. Kama Messi, Mkude,
Chanongo ni muhimu kwasasa katika timu, basi mafaniko haya yanatakiwa
kuwasukumu zaidi kuendeleza soka la vijana.
Kuna haja ya
kutafuta utamaduni wa mpira wa Simba ili kuwajenga wachezaji katika mfumo
mmoja. Na ili kufanikiwa, lazima pia waamue kuwaamini makocha na kuwapa muda
zaidi.
Tafuteni
walimu wanaoendana na mpira mtakaobuni katika klabu ya Simba ili wafanye kazi na vijana wenu kutengeneza
mpira rasmi wa Simba.
Leo Milovan,
kesho Liewig, keshokutwa kibadeni, mtondo Logarusic. Hapa mtakuwa mnajidanganya
tu.
Kaburu kwa
hili sina tatizo nawewe, nitakuunga mkono kwa ushauri pia.
0 comments:
Post a Comment