Jaja
akipokea nakala ya mkataba wake kutoka kwa Katibu Mkuu wa Young Africans Bw
Beno Njovu leo maraa baada ya kusaini kuitumikia kwa miaka miwili
Imechapishwa Julai 21, 2014, saa 7:31 mchana
HATIMAYE
mshamabuliaji Geilson Santos Santana "Jaja" raia wa Brazil leo
amesaini mkataba wa miaka miwili (2014-2016) kuitumikia timu ya Young Africans
kwa ajili ya michuano mbalimbali ikiwemo ya Ligi Kuu ya Vodacom pamoja na
mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika mwakani.
Katibu
mkuu wa Young Africans Bw Beno Njovu amesema usajli wa Jaja unakua ni wa
pili msimu huu kwa wachezaji wa kimataifa baada ya awali kumsajili kiungo
mshambuliaji Andrey Coutinho ambaye pia ni raia wa Brazil.
"Kazi
yetu uongozi ni kutekeleza maelekezo ya kocha mkuu pamoja na benchi la ufundi,
walitoa mapendekezo ya usajili kabla hawajaanza kazi na mengine baada kuwasili
yote tunajitahidi kuyatekeleza ili kila kitu kiende safi" alisema Beno.
Jaja
ambaye alizaliwa tarehe 21 Septemba 1985 na kukulia katika mji wa Aracaju
nchini Brazili mpaka anasajiliwa na timu ya Young Africans alikuwa akiichezea
timu ya Itabaina FC iliyopo nchini Brazil.
Mshambuliaji
huyo mwenye mwili uliojaa vizuri tayari alishaanza mazoezi tangu katikati ya
wiki iliyopita chini ya Kocha Mkuu Marcio Maximo na msaidizi wake Leonado Neiva
ambao wanaendelea kukinoa kikosi cha Young Africans kwa ajili ya michuano
mbalimbali.
Chanzo: Tovuti ya Yanga sc
0 comments:
Post a Comment