Imechapishwa Julai 31, 2014, saa 9:42 alasiri
LICHA ya kuboronga kombe la dunia majira ya
kiangazi mwaka huu nchini Brazil, Fabio Capello ataendelea kuwa kocha wa timu
ya taifa ya Urusi mpaka 2018 .
Waziri wa michezo wa nchi hiyo, Vitaly Mutko amemtania
kuwa kama atatwaa kombe la dunia lijalo, atazikwa sehemu aliyozikwa mwandishi
gwiji, Fyodor Dostoyevsky.
Muitaliano huyo aliiongoza nchi hiyo ya Ulaya
mashariki katika mashindano ya kombe la dunia, lakini alitupwa nje hatua ya
makundi ambapo alikuwa na timu za Ubelgiji, Korea Kusini na Algeria.
Hata hivyo, Capello ataendelea kuwa kocha mkuu
mpaka 2018 wakati ambao Urusi itakuwa mwenyeji wa fainali zijazo za kombe la
dunia na Vitaly Mutko anasema anayo nafasi ya kushinda mioyo ya watu wa Urusi.
“Kama tutafanikiwa kwenye mashindano ya mwaka
2018, tutamzika karibu na Dostoyevsky,” aliwaambia waandishi wa habari.
Wakati huo huo, Capello anajiandaa na michuano ya
mataifa ya Ulaya mwaka 2016, lakini amekiri kuwa kipaumbele chake ni fainali za
kombe la dunia 2018.
“Lengo kubwa ni kombe la dunia, lakini kwanza
tunatakiwa kufuzu michuano ya Ulaya mwaka 2016 nchini Ufaransa,” alisema.
0 comments:
Post a Comment