Imechapishwa Julai 30, 2014, saa 3:12 asubuhi
TIMU ya El Hilal ya Sudan imemfukuza kazi kocha
wake, Mbrazil, Paulo Compas kufuatia kitendo cha utovu wa nidhamu alichoonesha
mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo klabu hiyo ilipoteza mechi ya raundi ya nne
ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya AS Vita ya DR Congo.
Mechi hiyo wa ugenini iliyopigwa mjini Kinshasa,
Hilal waliweza kuwakomalia Vita kwa sare ya 1-1 mpaka dakika za mwisho, lakini
penati iliyotolewa na mwamuzi dakika za nyongeza ilimchukiza kocha Campos
aliyemshambulia mwamuzi wa mechi hiyo.
Mbrazil huyo aliingia uwanjani, akiwafuata
wachezaji wake ili wawashambulie waamuzi, kitendo ambacho Hilal ililaani
baadaye.
“Bodi imeamua kuvunja mkataba wa kocha Campos na
amepewa taarifa hiyo. Kocha anastahili kuwa mwalimu na atakakiwa kuonesha tabia
nzuri. Alifanya tofauti alipoingia uwanjani kumshambulia mwamuzi, akiwafuata
wachezaji wanaotakiwa kumuona kama mtu wa mfano kabla ya kuzuiliwa na polisi,”
Katibu mkuu wa El-Hilal, Emad Al-Tayeb alisema.
“Kitendo hicho kitaigharimu sana klabu na ndio
maana mkataba wake umevunjwa na kocha wake msaidizi, Al-Tag Mahgoub ataiongoza
timu mchezo ujao dhidi ya TP Mazembe. Pia tumetuma barua rasmi ya malalamiko kwenda
CAF kuhusu maamuzi ya refa katika dakika za mwisho,” alisema.
Hilal alipoteza mechi kwa mabao 2-1 na kwasasa
wapo nafasi ya tatu kundi A wakijikusanyia pointi 4 nyuma ya wacongo wenzao, TP
Mazembe.
0 comments:
Post a Comment