Imechapishwa Julai 28, 2014, saa 10:34 jioni
CRISTIANO Ronaldo ameshinda tuzo ya Goal 50 ya mchezaji bora wa
dunia baada ya kuwa na msimu mzuri wa 2013-14.
Mshambuliaji huyo ametwaa tuzo hiyo kwa mara ya tatu kama sehemu
ya kuheshimu kazi aliyoifanyia Real Madrid kutwaa taji la 10 la ligi ya
mabingwa barani Ulaya.
Nyota huyo mwenye miaka 29, pia alishinda kombe la mfalme (Copa
del Rey) na kufunga magoli 51 katika mashindano yote ya klabu na taifa lake.
WALIOSHINDA TUZO YA Goal 50 mpaka sasa:
2008- Cristiano Ronaldo
2009 -Lionel Messi
2010- Wesley Sneijder
2011-Lionel Messi
2012- Cristiano Ronaldo
2013 -Lionel Messi
2014 -Cristiano Ronaldo.
Ronaldo alishinda kiatu cha dhahabu sambamba na Luis Suarez na
mapema mwaka huu alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa dunia na kushinda tuzo ya 2013
FIFA Ballon d`Or.
Baada ya kupokea tuzo hiyo, Ronaldo alisema: “Ni heshima kubwa
kwangu kuchaguliwa kuwa mchezaji bora. Kiukweli nimefurahi sana”.
“Nashawishika kusema nisingeweza kutwaa tuzo hii bila sapoti
kutoka watu wa Real Madrid”.
Goal 50 ni moja ya tuzo za heshima kwenye mchezo wa soka
kwasababu wanaochagua wanatoka katika mitandao mikubwa ya soka duniani.
Kura zinapigwa baada ya kumalizika kwa misimu ya ligi za ndani
na mashindano ya kimataifa na wanaopiga kura wanatoka mataifa mbalimbali.
Zaidi ya waandishi wa habari 600 kutoka katika machapisho 35
wanachagua wachezaji 50 wa juu kwenye tuzo hiyo.
Ronaldo ameongoza mwaka huu akifuatiwa na Arjen Robben,
aliyeifanyia makubwa Uholanzi katika fainali za kombe la dunia na kuisaidia
klabu yake ya Bayern kutwaa makombe manne msimu wa 2013-14.
Mshindi wa mwaka jana, Lionel Messi alishika nafasi ya tatu baada ya msimu mbaya
katika klabu yake ya Barcelona na kushindwa kutwaa kombe la dunia nchini Brazil.
0 comments:
Post a Comment