Na Mwandishi Wetu, Tanga
TIMU ya Coastal Union ya Tanga "Wagosi wa Kaya" leo
inatarajiwa kucheza mechi ya kirafiki na African Sports “Wanakimanumanu” kwenye
uwanja wa CCM Mkwakwani itakayokuwa ya kusheherekea sikukuu ya iddi Pili.
Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema maandalizi
ya kuelekea mchezo huo yamekamilika kwa asilimia kubwa na
kinachosubiriwa na mechi hiyo itakayoanza saa kumi jioni kwenye uwanja huo.
El Siagi amesema baada ya kumaliza mechi hiyo timu hiyo
itaelekeza mipango yake ya kucheza mechi za kirafiki nyengine ili kuweza
kujiweka imara kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu soka Tanzania
bara.
Alisema wachezaji wa timu hiyo wataingia kwenye mechi hiyo kwa
malengo ya kupata ushindi ili kuweza kuendeleza rekodi ya kuwafunga
wanakumanumanu hao ambao msimu ujao watashiriki michuano ya ligi daraja la
kwanza.
Kwa upande wake,Ofisa Habari wa timu ya African
Sports,Wanakimanumanu” Said Karsandas alisema kuwa wamepania kushinda kwenye
mechi hiyo ili kuweza kurudisha ile heshima ya timu hiyo kwa wagosi hao wa
kaya.
“Tunajua mechi hii itakuwa ni ngumu kutokana
na uwezo wa Coastal Union hivyo nasi tumejipanga kuweza kufanya vizuri ili
kutoa burudani kabambe “Alisema Karsandas.
Hata hivyo aliwataka wakazi wa mkoa wa Tanga na viunga vyake
kujitokeza kwa wingi kushuhudia burudani itakayokuwa ikitolewa kwenye mechi
hiyo .
0 comments:
Post a Comment