Imechapishwa Julai 25, 2014, saa 2:49 usiku
KOCHA wa zamani wa Chelsea, Claudio Ranieri ameteuliwa kuwa kocha mpya wa timu ya Taifa ya Ugiriki.
Ranieri katika miaka kumi iliyopita amevuna zaidi ya paundi milioni 10, akilipwa kama fidia ya kufukuzwa kazi, lakini Ugiriki umemteua kuwa kocha mkuu wa nchi hiyo.
Ranieri amesaini mkataba wa miaka miwili na anatarajiwa kulibadili soka la nchi hiyo.
Kocha huyo amefukuzwa mara tano (5) katika miaka 10 iliyopita na kuvuna fidia kubwa ya paundi milioni 10.
Ilifukuzwa kazi na klabu za Chelsea, Valencia, Inter Milan, Juventus na Monaco baada ya kuvurunda mno.
Licha ya kuwa na rekodi mbovu katika historia ya kushinda makombe, kocha huyo mwenye miaka 62 bado anaendelea kupata kazi nzuri zenye ulaji wa kutosha.
Alilipwa paundi milioni 4 mwezi mei baada ya kufukuzwa kazi katika klabu ya Monaco.
Akiwa Chelsea alipewa jina la utani la 'Tinkerman` kutokana na mfumo wake wa kubadili kikosi mara kwa mara.
Changamoto ya Ugiriki: Claudio Ranieri anatarajia kuiongoza nchi hiyo katika fainali za mataifa ya Ulaya mwaka 2016
Mzee wa kufukuzwa: Ranieri siku za karibuni amevunjiwa mkataba na Monaco na kuvuna paundi milioni 4 kama fidia.
Uzoefu wa kutosha: Claudio Ranieri siku za nyuma aliziongoza klabu za Chelsea na Juventus
Alifukuzwa Chelsea mwaka 2004 na kocha huyo mwenye miaka 62 amevuna paundi milioni 10 kama fidia baada ya kufukuzwa katika klabu nne ndani ya miaka 10.
Wakati Ranieri anafukuzwa na Roman Abramovich mwaka 2004, bado alikuwa na miaka mitatu katika mkataba wake darajani ambapo angevuna paundi miliobi 2 kama malipo ya mshahara.
Alishutumiwa kwa tabia yake ya kubadili kikosi na alipewa jina la utani la 'Tinkerman, lakini mwaka huo akiwa anafanya kazi, Chelsea alishika nafasi ya pili na kufika nusu fainali ya UEFA.
Mafanikio hayo hayakutosha kwa Abramovich, ambaye alikuwa tayari kumlipa fidia kutokana na kumfukuza kazi kwasabau aliona kama ameshindwa kutimiza malengo.
Chelsea ililipa fidia iliyokaribia paundi milioni 1 na bosi huyo aliondoka kwenda Valencia kurithi mikoba ya Rafa Benetiz aliyeteuliwa kuwa kocha wa Liverpool.
Katika miezi nane ya kazi nchini Hispania, alianza kutafuta kazi baada ya kuvurunda akiwa na Valencia.Viongozi walichukizwa sana na timu yao kutolewa katika mashindano ya UEFA dhidi ya Steaua Bucharest na kuamua kumfukuza kazi na alitoka na mkwanja wa kutosha.
Inaaminika kuwa Ranieri alivuna mzigo wa paundi milioni 4 baada kufukuzwa kazi, na ilimchukua miaka miwili kutulia kabla ya kupata kazi mpya.
Ranieri (kushoto) alipewa jina la utani la 'Tinkerman' akiwa katika klabu ya Chelsea kutokana na tabia yake ya kubadili kikosi mara kwa mara.
0 comments:
Post a Comment