Geilson Santos Santana
Imechapishwa Julai 15, 2014, saa 12:12 jioni
Mshambuliaji
wa kimataifa kutoka nchini Brazil Geilson Santos Santana "Jaja"
amewasili leo mchana jijini Dar es salaam akitokea jijini Sao Paul tayari kwa
kuanza kazi ya kuitumikia klabu ya Young Africans Sports Club kwa msimu wa
2014/2015.
Jaja
ambaye alikua akichezea timu ya Itabaina FC nchini Brazil, anakuwa ni mchezaji
wa pili kuungana na kikosi cha Young Africans baada ya Andrey Coutinho kuwa
mchezaji wa kwanza kujiunga na kikosi cha kocha Marcio Maximo.
Usajili
wa wachezaji hawa ni muendelezo wa uongozi wa Young Africans kuhakikisha msimu
ujao unakua na kikosi bora ambacho kitaweza kufanya vizuri kwenye michuano ya
Ligi Kuu ya Vodacom na mashindano ya Kombe la Shrikisho Barani Afrika.
Jaja
anaungana na makocha wabrazil Marcio Maximo na Leonardo Neiva na kiungo Andrey
Coutinho katikaa msimu huu ambapo kwa pamoja ushirikiano wao na wachezaji
wengine wazawa wataisaidia Young Africans kufanya vizuri.
Kesho
asubuhi Jaja anatarajiwa kuanza mazoezi katika shule ya sekondari Loyola ikiwa
ni sehemu ya maandaliz ya michuano mbalimbali itayowakabili.
Chanzo:Tovuti ya Yanga sc
0 comments:
Post a Comment