|
|
Enner Valencia akiwa na timu ya taifa ya Ecuador katika mchezo dhidi ya Honduras. |
Na Alwaatan R. Ngoda
Imechapishwa Julai 13, 2014, saa 08:47 mchana
Kocha wa klabu ya West Ham United, Sam Aladyce 'BIG SAM' amemuomba mwenyekiti wa klabu hiyo David Sullivan kuangalia uwezekano wa kumpata mshambuliaji wa klabu ya Pachuca na timu ya taifa ya Ecuador, Enner Valencia aliyeonesha kiwango cha hali ya juu na timu ya taifa katika michuano ya kombe la dunia licha ya kuondoshwa mapema kwa timu yake ya taifa.
kocha wa West Ham United, Sam Aladyce 'BIG SAM' akiwa katika 'pozi la kazi' |
Aladyce amedhamiria kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu soka nchi Uingereza na anaona ujio wa Valencia utakuwa na tija katika kikosi hicho cha wagonga nyundo wa jiji la London.
Kama Valencia atafanikiwa kutua Upton Park atakuwa ni mchezaji watano kusajiliwa na West Ham katika kipindi hiki cha usajili kwani tayari wachezaji kama Mauro Zarate, Cheikhou Kouyate, Aaron Cresswell na Diego Poyet wamekwishamwaga wino kuitumikia klabu hiyo.
Enner Remberto Valencia Lastra (25), amepachika wavuni mabao 18 katika mechi 23 alizoichezea Pachuca inayoshiriki ligi kuu nchini Mexico na mambo yakienda sawia anaweza tuwa West Ham kwa uhamisho utakaowagharimu"hummers" kiasi cha pauni milioni 12
Kocha Sam Aladyce ana matumaini ya kumnasa mshambuliaji huyo ndani ya siku tatu zijazo na hatimaye kujumuika naye katika ziara yao ya nchini New Zealand wiki ijayo kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.
Valencia alifunga bao lake la kwanza kwa timu ya taifa ya Ecuador almaarufu 'La tri' katika michuano ya kombe la dunia kwenye mchezo dhidi ya Switzerland katika dimba la 'Estadio Nacional Mane Garrincha' jijini Brasilia walipokubali kichapo cha mabao 2-1, akifunga pia mabao yote mawili katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Honduras katika mchezo wa pili.
'Big Sam' angependa kuwa na safu kali zaidi ya ushambuliaji itakayomjumuisha Valencia, Matt Jarvis, Stewart Downing na wengine ndani ya West Ham iliyomaliza nafasi ya 13 katika msimamo wa ligi kuu nchini humo msimu uliomalizika wa 2013/14.
0 comments:
Post a Comment