Kutoka kulia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Saidy Meckysadick, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi,
Farough Baghozah na Wajumbe, Evarist Hagila na Saad Kawemba
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
Imechapishwa Julai 24, 2014, saa 1:23 usiku
MAANDALIZI ya ziara ya magwiji wa Real Madrid ‘Real
Madrid Legends’ yamezidi kushika kasi ambapo leo kamati ya maandalizi imemtembelea
mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Saidy Mecky Sadick, ofsini kwake, Ilala Jijini
Dar kwa lengo la kumueleza rasmi tukio hilo la kihistoria litakalofanyika mwezi
ujao.
Kamati hiyo ikiongozwa na mwenyekiti wake, Farough
Baghozah ilikutana na mkuu huyo wa mkoa ambaye alifurahiswa na jambo hilo
litaloweza kufungua fursa mbalimbali ikiwemo kuutangaza utalii wa Tanzania anga
za kimatifa.
Menenja wa ziara hiyo, Dennis Ssebo amesema kwamba
walikaribishwa kwa heshima na mkuu wa mkoa na kuahidi kuwapa ushirikiano
mkubwa, huku akiwa mwenyeji wa magwiji hao wanaokuja kwa mara ya kwanza barani
Afrika.
“Tumepokelewa vizuri na mkuu wa mkoa.
Umetukaribisha kwa heshima zote na ameahidi kutupa ushirikiano mkubwa,” Alisema
Ssebo.
Magwiji hao watatua nchini Agosti 22 mwaka huu na
kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya kikosi maalum cha nyota wa Tanzania Agosti
23 uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Ssebo alisema mechi hiyo itatazamwa kwa kiingilio
cha chini kabisa cha shilingi elfu tano na wanaamini watanzania wengi wataweza
kumudu kwasababu wamepewa taarifa mwezi mmoja kabla.
Miongoni mwa wachezaji hao waliopata kutamba
katika michuano ya La Liga, UEFA na kombe la dunia ambao watatua nchini ni
pamoja na Luis Madeila Figo, Zidedine Zidane, Fabio Cannavaro, Roberto Carlos ,
Ronaldo de Lima, Michael Owen na wengineo.
Baada ya mechi ya kirafiki, magwiji hao
watatembelea vivutio mbalimbali vya utalii hapa nchini na kupanda Mlima
Kilimanjaro, jambo ambalo litaonwa na watu wengi zaidi duniani kwasababu hata Real
Madrid TV itakuwepo kurekodi tukio zima.
Ujio wa magwiji hao ni mwaliko wa kampuni ya
Tanzania Sisi ni Nyumbani (TSN), chini ya Mkurugenzi wake, Farough Baghozah.
Vodacom Tanzania ni miongoni mwa makampuni
yaliyojitokeza kudhamini ziara hiyo. Makampuni mengine ni Fastjet, Tropical,
Pembe Flower, Lake Gas, EFM Radio na Ladger Plaza Bahari Beach.
Hata hivyo nafasi ya kudhamini bado ipo, waratibu
wa ziara hiyo wanatoa wito kwa makampuni na taasisi mbalimbali kujitokeza
kudhamini kwasababu ni fursa kubwa ya kujitangaza kitaifa na kimataifa.
0 comments:
Post a Comment