Tatizo likaanza: Seydou Keita (wa pili kushoto) aligoma kupokea mkono wa Pepe (wa nne kushoto).
Imechapishwa Julai 30, 2014, saa 7:38 mchana
MSIMU bado haujaanza, lakini tayari dunia imeanza kuzungumzia upinzani wa Real Madrid na Barcelona.
Lakini wakati huu klabu ya Katalunya haijahusika-kiukweli, hisia mbaya zimekuja katika mchezo wa maandalizi ya kabla ya msimu baina ya Real Madrid na nyota wa zamani wa Barca.
Mchezaji wa Roma, Seydou Keita aligoma kusalimiana na beki wa Ureno, Pepe na kumrushia chupa ya maji kabla ya mechi hiyo ya kirafiki kuanza.
Tulia: Mchezaji mwenzake akijaribu kumtuliza kiungo huyo wa Mali, lakini haikusaidia kitu.
Mchezaji mwenzake na Keita akijaribu kumuondoa kwenye eneo la tukio baada ya wachezaji wa Real Madrid kuanza kulalamika
Bifu: Keita alimrushia chupa ya maji Pepe (juu kabisa kulia) na kumlowanisha.
Acha hizo!: Pepe (wa pili kulia) avumilivu ulimshinda baada ya chupa ya maji kutua karibu yake na akarudi kulianzisha.
Pia inasemekana Pepe alikuwa na mzozo na Keita wakati wa mechi, lakini hawakunaswa na kamera.
Haya yalitokea katika ushindi wa bao 1-0 wa Roma dhidi ya mabingwa hao wa Ulaya, jumatano asubuhi katika mchezo wa kombe la kimataifa la Guinness mjini Dallas.
Pepe na Keita walikuwa na bifu miaka ya nyuma kwenye mechi za El Clasico na walipokutana tena wameliendeleza.
Wawili hao wana historia: Keita alimtuhumu Pepe kuwa alimuita nyani kwenye mechi ya El Clasico ya Supercopa mwaka 2011.
Historia: Keita na Pepe hawakuwa marafiki ambapo mchezaji huyo wa zamani wa Barca alimtuhumu mwenzake kwa kumuonesha ubaguzi wa rangi.
Safari hii baada ya Keita kugoma kumsalimia mpinzani wake kabla ya mechi, walitenganishwa na wachezaji wenzao, ambapo Iker Casillas na Xabi Alonso walikuwa wapatanishi wa amani.
Hasira: Keita bado anaonekana kuwa na hasira wakati ikiongea na mchezaji wa Real Madrid, Isco baada ya tukio hilo.
0 comments:
Post a Comment