BEKI wa Manchester United, Rafael,
atakosa mechi zilizosalia za klabu hiyo katika ziara ya maandalizi ya kabla ya
msimu nchini Marekani baada ya kupata majeruhi ya nyonga.
Beki huyo wa pembeni wa Brazil mwenye
miaka 24 alipata majeruhi hayo katika ushindi wa Man United wa mabao 3-2 dhidi
ya Roma siku ya jumamosi.
Ingawa ukubwa wa tatizo haujulikani,
lakini taarifa hizo ni mbaya kwa kocha Louis Van Gaal ambaye anatarajia kutumia
zaidi mabeki wa pembeni kupandisha mashambulizi msimu ujao.
Mholanzi huyo amewapoteza Rio
Ferdinand, Nemanja Vidic na Patrice Evra waliotimka Old Trafford, na hii itampa
wakati mgumu katika mfumo wake wa 3-4-1-2 ambao anawatumia mabeki watatu
katikati.
Rafael alitarajiwa kucheza beki ya
kulia ambayo Antonia Valencia ilikuwa anatumika kutokana na kukosa beki
mwingine wa kulia.
Phil Jones na Chris Smalling walitumika
kuziba nafasi ya Mbrazil huyo msimu uliopita, lakini kwasasa ndio mabeki watatu
pekee wa kati wenye uzoefu waliosalia klabuni.
Rafael atakuwa anapata matibabu kwenye
kambi ya klabu hiyo mjini Manchester na anatarajia kuungana na wenzake baadaye
majira haya ya kiangazi.
“Rafael amerudi Manchester kuendelea
na matibabu kufuatia majeruhi ya nyonga aliyoyapa wakati za mazoezi uwanja wa
Denver”. Ilisema taarifa ya United iliyochapishwa kwenye mtandao wake rasmi.
0 comments:
Post a Comment