Wilfried Zaha na beki wa zamani wa United Nemanja Vidic wakichuana.
Imechapishwa Julai 31, 2014, saa 4:29 asubuhi
WINGA wa Manchester United , Wilfried Zaha amesema anatarajia kuwa mchezaji wa aina aitakayo Louis Van Gaal baada ya msimu uliopita kutoswa na aliyekuwa kocha wa timu hiyo David Moyes.
Zaha alitoshwa na kocha Moyes na kumtoa kwa mkopo katika klabu ya Cardiff mwezi januari kwa madai kuwa nyota huyo ana mitazamo mibaya.
Kinda huyo mwenye miaka 21, sasa amepewa nafasi ya kuonesha uwezo wake kwa Van Gaal na katika mechi ambayo Man United ilishinda kwa penati dhidi ya Inter Milan, kocha huyo alimwacha Zaha mpaka kipindi cha pili ili aoneshe ujuzi wake katika mechi yake ya kwanza ya maandalizi ya kabla ya msimu.
Zaha alipewa nafasi ya kumuonesha uwezo kocha Van Gaal kwenye mechi dhidi ya Inter Milan.
Van Gaal amemuambia Zaha kuwa anatakiwa kujitahidi kuwa mshambuliaji wa kati ili aingie katika mfumo wake wa 3-5-2 msimu ujao.
Zaha alisema: "Nilikuwa nacheza winga, lakini kama kocha anataka nizoee nafasi nyingine, nitafanya,"
"Sio kwamba mimi naweza winga tu, nitacheza nafasi nyingine".
"Nimesikia anataka kuwapa nafasi wachezaji vijana. Hiki ndicho nilihitaji tangu nimefika hapa. Nataka kuwa mchezaji wa Man United. Natumaini kupata nafasi msimu ujao".
Sir Alex Ferguson alimnunua Zaha januari mwaka 2013 kutokea klabu ya Crystal Palace.
0 comments:
Post a Comment