Imechapishwa Julai 23, 2014, saa 5:43 asubuhi
BAADA ya likizo ya baada ya kombe la dunia, Joel Campbell muda wowote anajiunga na klabu yake ya Asernal kwa maandilizi ya kabla ya msimu.
BAADA ya likizo ya baada ya kombe la dunia, Joel Campbell muda wowote anajiunga na klabu yake ya Asernal kwa maandilizi ya kabla ya msimu.
Campbell aliyeifanyia Costa Rica mambo makubwa katika fainali za kombe la dunia nchini Brazil mwaka huu, aliposti picha kwenye mtandao wake wa Twita akiwa na demu wake mjini Paris.
Mshambuliaji huyo mwenye miaka 22 alisaini mkataba na Asernal mwaka 2011 na sasa anarudi London ambapo atapata nafasi ya kupigania namba katika kikosi cha kwanza cha Aserne Wenger.
Campbell alilazimika kuondoka kwa mkopo katika klabu ya Asenal kutokana na kupata matatizo ya kutokuwa na kibali cha kufanya kazi msimu uliopita.
Mwishoni mwa wiki, Campbell alitweet kuwa yuko njiani kupigania ndoto zake, akieleza kuwa ana nia ya kuingia katika kikosi cha Wenger.
Campbell aliposti picha akiwa na demu wake wakati huu yupo katika mapumziko ya baada ya fainali za kombe la dunia.
Mwaka jana, Campbell alikuwa na msimu mzuri nchini Ugiriki ikiichezea klabu ya Olympiacos na tayari Wenger amesema hataongeza tena mshambuliaji majira haya ya kiangazi, hivyo kuna nafasi ya Campbell Emirates.
Campbell anatarajia kuwepo katika kikosi cha Asernal kinachoenda leo mjini New York kwaajili ya mechi ya kujipima uwezo kabla ya msimu dhidi ya timu ya Thierry Henry ya New York Red Bulls siku ya jumamosi.
Alexis Sanchez, aliyesajiliwa kwa dau la paundi milioni 30 majira haya ya kiangazi atajiunga na wenzake wiki ijayo.
Joel Campbell ameonesha kuwa yeye ni hatari baada ya kuonesha soka maridadi kwenye fainali za kombe la dunia na sasa anaweza kuwa silaha ya Aserne Wenger.
Campbell akishangilia baada ya kufunga bao kwenye mechi dhidi ya Man United mwezi februari kwenye michuano ya UEFA
Campbell akishangilia baada ya kufunga goli dhidi ya Uruguay katika mechi ya kombe la dunia.
0 comments:
Post a Comment