Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
Imechapishwa Julai 30, 2014, saa 2:42 usiku
BAADA ya mapumziko ya siku mbili ya sikukuu ya Eid
El Fitri, mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara, wana Lambalamba, Azam fc
kesho wanaendelea na mazoezi ya kujiwinda na michuano ya ligi kuu pamoja na
ligi ya mabingwa barani Afrika katika uwanja wa Azam Complex, Mbande, Chamazi,
nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
Meneja wa Azam fc, Jemedari Said amesema wachezaji
wote wanajua hilo na kesho kocha mkuu, Mcameroon, Joseph Marius Omog na kama
mambo yatakwenda vizuri siku ya ijumaa wanatarajia kuwa na mechi ya kirafiki
dhidi ya timu ya ligi daraja la kwanza.
“Mechi za kirafiki zimekuwa zikimsaidia mwalimu
kwa kiasi kikubwa kuangalia maendeleo ya wachezaji wapya walioingia. Tuna
wachezaji 9 ambao wapo timu ya Taifa na wawili Majeruhi. Kwahiyo kuanzia wiki
ijayo baada ya kuiwakilisha nchi watajiunga na timu”. Alisema Jemedari.
“Mwalimu anasema mechi za kirafiki zimekuwa na
manufaa kwa wachezaji wapya kama vile Didier Kavumbagu, Ismail Diara ambao wanaendelea
vizuri sana,”
“Mwalimu ameniambia binafsi kuwa ataendelea na
mechi za kirafiki ili kuangalia kikosi chake, na hapo baadaye ataangalia
uwezekano wa kupata mechi za kirafiki za kimataifa kwa ukanda wa Afrika
mashariki au mbali zaidi,”
Kuhusu michuano ya Kagame, Jemedari alisema mpaka
sasa hawajapata taarifa rasmi ya CECAFA kama watashiriki baada ya awali kuambiwa
wataalikwa kwa nafasi ya upendeleo.
Hata hivyo alisema kocha Omog anaisubiri nafasi
hiyo na kama ataipata itamsaidia kupata maandalizi mazuri, lakini kama
haitatokea, ataangalia mechi za kirafiki.
0 comments:
Post a Comment