Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
Imechapishwa Julai 24, 2014, saa 1:38 usiku
MABINGWA wa ligi kuu soka Tanzaania bara, Azam fc
wamegonga mwamba kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya wagonga nyundo wa Mbeya,
Mbeya City ikiwa ni sehemu ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu unaotarajia
kuanza kushika kasi Saptemba 20 mwaka huu.
Afisa habari wa klabu hiyo, Jafar Idd Maganga
alisema wamewasiliana na kocha mkuu wa Mbeya City fc, Juma Mwambusi kuomba
kucheza mechi ya kirafi mkoani Mbeya au Chamazi, lakini imeshindikana kwasababu
wao wameamua kupumzika.
“Tumewasiliana na Mwalimu Mwambusi kuomba kucheza
nao mechi ya kirafiki, lakini imeshindikana kwasababu ametueleza kuwa baada ya
ligi kusogezwa mbele wameamua kupumzika. Kwahiyo hawaendelei na mazoezi”.
Alisema Jafar.
“Tunacheza mechi za kirafiki kwa lengo la kocha mkuu
Joseph Marius Omog kutazama kama wachezaji wake wanaelewa mafundisho yake”.
Azam ambao leo hii asubuhi walishinda bao 1-0
dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa kirafiki uliopigwa uwanja wa Chamazi
wamedhamiria kuomba mechi ya kirafiki na wekundu wa Msimbazi Simba.
Jafar alisema tayari wameshaongea na makamu wa Rais
wa Simba, Geofrey Nyange` Kaburu` na amewaambia atatoa jibu siku chache zijazo.
“Kama kuna uwezekano tunataka kucheza na Simba,
Tumeshaongea na Kaburu na kutueleza kuwa atatujibu. Kama watakuwa tayari, sisi
tuko tayari muda wowote kucheza nao”. Alisema Jafar.
0 comments:
Post a Comment