Imechapishwa Julai 26, 2014, saa 6:46 mchana
BOSI
wa Asernal, Mfaransa, Aserne Wenger amefichua siri kuwa alikaa kwa kirefu na
Aaron Ramsey kwa lengo la kuzungumza naye ili kunusuru kiwango cha nyota huyo
wa Wales.
Majeruhi
ya mfululizo iliathiri sana kiwango cha nyota huyo mwenye miaka 23, lakini
alionekana kuwa msaada katika klabu ya Asernal wakati wa harakati zake za
kumaliza ukame wa miaka 9 bila kikombe msimu uliopita.
Baada
ya kukaa chini na kocha wake, Ramsey aliibuka tena na kuwa moja ya wachezaji
nyota wa ligi kuu msimu uliopita, akifunga mabao 16 na kuisadia Asernal kutwaa
kombe la FA.
“Nilikaa
chini na Aaron na nilimwambia, ‘Sidhani kama watu hawakupendi, lakini hawapendi
mchezo wako kwa wakati huu’, Mfaransa huyo alieleza wakati wa ziara yao ya
maandalizi ya kabla ya msimu nchini marekani.
“Alitakiwa
kurejea katika mchezo wake….halafu ulimuona mchezaji tofauti, kwasababu ana
akili, na baada ya kutoka katika mazungumzo, nilijua kijana ataweza kurudi upya”.
Ramsey
alianza katika ushindi wa Asernal wa mabao 2-0 dhidi ya Boreham Wood, ukiwa ni
mchezo wao wa kwanza wa kirafiki wakati huu wa maandalizi ya kabla ya msimu, na
anatarajiwa kucheza dhidi ya New York Red Bulls siku leo jioni.
0 comments:
Post a Comment