Kiungo mwalimu: Kiwango alichoonesha Sami Khedira katika fainali za mwaka 2014 za kombe la dunia kimewavutia wengi.
Imechapishwa Julai 14, 2014, saa 9:11 alasiri
ASERNAL wamejiandaa kuwapiga bao Chelsea kwa kumsajili kiungo wa Ujerumani, Sami Khedira kutoka klabu ya Real Madrid.
Magazeti ya Hispania yunaripoti kuwa dili hilo la paundi milioni 23 limeshakubaliwa.
Kwa mujibu wa Sport, Khedira atasaini mkataba wa miaka minne katika dimba la Emirates, licha ya Chelsea kujitokeza kuitaka saini ya mtaalamu huyo.
Mazungumzo ya mkataba mpya baina ya wawakilishi wa nyota huyo mwenye miaka 27 na Real Madrid yalivunjika, hivyo kilichobaki ni kumuuza majira haya ya kiangazi.
Amezama kwenye busu: Khedira akishangilia ubingwa wa Ujerumani katika dimba la Maracana.
Kwenye rada: Khedira alifunga bao katika mechi ya nusu fainali baina ya Ujerumani dhidi ya Brazil
Tayari Asernal wameshatumia paundi milioni 30 kumnunua mshambuliaji wa Chile, Alexis Sanchez kutokea klabu ya Barcelona, na wamefanikiwa kumsajili beki wa kulia wa Ufaransa katika fainali za kombe la dunia, Mathieu Debuchy kutoka klabu ya Newcastle.
Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho, aliyefanya kazi na Khedira wakati akiwa Real Marid yuko makini kumsajili kiungo huyo wa ulinzi, lakini anaonekana atamkosa.
Khedira alikosa mechi ya fainali jana jumapili baada ya kupata majeraha wakati akiwa mazoezini.
Hata hivyo, alijumuika na wenzaka katika sherehe za ubingwa baada ya Ujerumani kuipiga Argentina bao 1-0 na kutwaa kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil.
0 comments:
Post a Comment