Katibu wa Baraza la Wazee wa klabu ya Yanga SC
Mzee Ibrahim Akilimali akiongea na waandishi wa habari leo makao makuu ya klabu.
Na Mwandishi Wetu
Imechapishwa Juni 11, 2014, saa 11:09 jioni
Baraza la Wazee wa Klabu ya Young Africans leo
wamefanya mkutano na waandishi wa habari makao makuu ya klabu na kuwakemea wanachama
wanaosema ya kwamba watapeleka barua TFF kwa ajili ya kuushitaki uongozi kuwa
wamevunja Katiba kwa kuongeza muda wa mwaka mmoja kuwa madarakani.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya
klabu, Katibu wa Baraza la Wazee Bw Ibrahim Akilimali amesema kwa niaba ya
Baraza la Wazee wanasema wanachama wanaopinga maamuzi ya mkutano mkuu uliokuwa
na wanachama zaidi ya 1500 basi wafuate taratibu za kuwasilisha malalamiko yao
ni si kufanya vinginevyo.
"Mwenyekiti wetu Yusuf Manji alishasema tangu
mapema ya kwamba yeye hatagombea tena na siku ya mkutano aliyasema hayo awali,
lakini Mjumbe wa Baraza wa Wadhamini mzee Jabir Katundu aliwasilisha hoja ya
kumuomba aendelee na uongozi, ndipo wanachama walipopata nafasi ya kujadili
chini ya Mama Karume na kwa pamoja kuafiki Mwenyekiti aendelee japo kwa miaka
minane "alisema Akilamali.
Aidha Akilimali alisema Manji hakuafikiana na
suala hilo na ndipo alipoomba japo aongezewe muda wa mwaka mmoja kabla ya
kuelekea kwenye mikikimikiki ya Uchaguzi ili aweze kukamilisha baadhi ya mambo
kama ya usajili, ujio wa kocha mkuu mpya Marcio Maximo na ujenzi wa Uwanja.
Naye mwenyekiti wa Baraza la Vijana Bw Bakili
Makele amesema wao kama vijana pia wanashangazwa hao baadhi ya wanachama ambao
wanataka kuirudisha Yanga nyuma, mara hii wameshasahau shuruba tulizopitia
mpaka kufikia muafaka, sisi kama vijana tunasema hatuamini kama hao wanaosema
hawakubaliani na maamuizi ya mkutano ni watu wanaoitakia mema klabu yetu.
"Mwenyekiti Bw Yusuf Manji hajayapenda
madaraka na wala haitaji kuendelea kuiongoza Yanga, bali kwa maombi yetu sisi
wanachama pamoja na Baraza la Wadhamini alikubali kuiongoza japo kwa mwaka
mmoja kabla ya kuelekea kwenye mkutano mkuu wa Uchaguzi ambapo atakayejiona ana
uwezo wa kuongoza Yanga basi atapata fursa hiyo ya kujinadi na si kupiga kelele
sasa hivi kweye vyombo vya habari" alisema Bakili.
0 comments:
Post a Comment