Na Boniface Wambura, Dar es salaam
Imechapishwa Juni 2, 2014, saa 6: 11 mchana
Kikosi
cha Taifa Stars ambacho jana (Juni 1 mwaka huu) kiliitupa Zimbabwe (Mighty
Warriors) nje ya michuano ya Afrika baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 kinarejea
nchini leo (Juni 2 mwaka huu) kutoka Harare.
Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itatua Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam saa 12.30 jioni kwa
ndege ya Kenya Airways ikitokea Harare kupitia Nairobi.
Stars
imefuzu kucheza raundi inayofuata kwa ushindi wa jumla ya mabao 3-2, kwani
awali (Mei 18 mwaka huu) iliifunga Zimbabwe bao 1-0 katika mechi ya kwanza
iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika
raundi ya pili, Taifa Stars itacheza na Msumbiji ambapo itaanzia nyumbani kati
ya Julai 19 na 20 mwaka huu, wakati mechi ya marudiano itafanyika Msumbiji kati
ya Agosti 2 na 3 mwaka huu.
Wakati
huo huo, Taifa Stars imeendelea kupokea salamu za pongezi kutoka kwa wadau
mbalimbali baada ya kufanikiwa kuvuka kikwazo hicho cha kwanza katika harakati
zake za kucheza Fainali za Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Morocco.
Salamu
hizo zimetoka kwa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya (MREFA), Chama cha
Mpira wa Miguu Mkoa wa Manyara (MARFA), mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) akiwakilisha Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa
Mwanza (MZFA), John Kadutu, na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Ahmed Idd Mgoyi.
WAKATI HUO HUO U15 TANZANIA
YATUA MEDALI VIFUANI
Timu
ya Tanzania ya wachezaji wenye umri chini ya miaka 15 iliyoshika nafasi ya pili
katika Michezo ya Afrika kwa Vijana (AYG) iliyofanyika Gaborone, Botswana
inawasili leo (Juni 2 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
U15
ambayo imeshinda mechi tatu, sare moja na kufungwa moja inawasili Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 12.30 jioni kwa ndege ya Kenya
Airways ikitokea Gaborone kupitia Nairobi.
Tanzania
ambayo imepata medali za fedha kwa kushika nafasi hiyo ikiwa chini yaKocha Abel
Mtweve ilizifunga Afrika Kusini 2-0, Botswana 2-0, Swaziland 3-0 na ikatoka
sare ya bao 1-1 na Mali. Ilifungwa mabao 2-0 na Nigeria ambao ndiyo walioibuka
mabingwa.
Wachezaji
16 waliounda kikosi cha Tanzania ni Adam Shayo, Amani Ally, Amos Manguli, Amri
Nyuki, Amede Amani, Baraka Rashid, David Uromi, Goodlove Mdumule, Hance Msonga,
Kelvin Kamalamo, Makalius Amrin, Nasson Chanuka, Paulo Ngowi, Petro Shaban,
Rajab Mohamed na Thomas Chindeka.
0 comments:
Post a Comment