Mwenyekiti
wa Klabu ya Young Africans Bw Yusuf Manji amesema wanachama wanaopinga
maamuzi ya mkutano mkuu uliofanyika Juni Mosi 2014 katika Bwalo la
Polisi Osyterbay ya kuwaongezea muda wa mwaka mmoja, wafike makao makuu
ya klabu na kujiorodhesha majina yao kwa Katibu Mkuu.
Akiongea
na waandishi wa habari makao makuu ya klabu, Manji amesema sisi sote
tunajenga nyumba hatuna haja ya kugombania fito, wanaopinga maamuzi
yale ni vyema wakajiorodhesha majina yao ili kuweza kupata idadi yao na
kama itafikia idadi ya waliohudhuria mkutano ule watu 1522 basi
tutaitisha mkutano mwingine.
Vyombo
vya Habari vimekua vikiripoti kuwa baadhi ya wanachama hawakubaliani na
maamuzi ya mkutano mkuu, na mie ni mfuata Demokrasia namuagiza Katibu
Mkuu kuweka reja hapa makao makuu kwa siku 5 kuanzia jumatatu mpaka
ijumaa saa 11 jioni hivyo wale wote wanaosema/wanaopingana na maamuzi ya
mkutano mkuu wapate kujioorodhesha.
Pili
kwa yoyote ambaye anaona anaweza kuiongoza Yanga kwa sasa milango iko
wazi, anaweza kufika makao makuu na kuongea na katibu mkuu kisha anaweza
kunadi sera zake/kuongea na waandishi wa habari na baadae tutapeleka
jina lake kwa Bodi ya Wadhamini wakiridhika nitaitisha mkutano mkuu wa
Uchaguzi.
Zoezi
la kujiorodhesha wanachama makao makuu litakua na usalama wa kutosha
kutoka kwa jeshi la Polisi ambapo patakua na askari wa usalama watakao
kuwa wakilinda usalama wa wanachama wanaofika kujiorodhesha kwenye reja
hiyo.
Jumamosi
ijayo Katibu Mkuu atatoa ripoti ya idadi ya wanachama walijiorodhesha
kwenye reja na kama idadi ifikia 1522 kama ya waliohudhuria mkutano mkuu
basi uongozi utaitisha upya mkutano mkuu, na kama idadi yao haitafikia
baadhi demokrasia itatawala kwa kufuata maamuzi ya watu wengi.
Chanzo: Tovuti ya Yanga
Chanzo: Tovuti ya Yanga
0 comments:
Post a Comment