Na Baraka Mbolembole
Narudia tena kusema; ‘ Mtu mkubwa ni Mwanafunzi’, na maana alisi ya neno falsafa ni ‘ Kutafuta busara, kupenda hekima’. Falsafa linatokana na maneno mawili ya Kiyunani; ‘ Philo’ lenye maana ya ‘ Upendo juu ya jambo fulani’ na ‘ sophia’ lenye maanaya ‘ busara’.
Nyakati za kale za kirumi, mwanafalsafa alikuwa ni mtu yeyote ambaye alionesha ubingwa wa kutafakari kwa busara na hekima masuala mbalimbali.
Katika nyakati za sasa neon falsafa hutumika kuelezea mtu anayefikiri kimantiki. Falsafa ni kutafuta –busara-hekima. Kila mmoja anaweza
kufikiri kwa namna yake na kusema lolote kuhusu uamuzi wa wanacha wa klabu ya Yanga kuachana na ajenda kuu ya marekebisho ya katiba ya klabu na kutumia muda mwingi katika mkutano mkuu kumuomba mwenyekiti aliyekuwa akitakiwa kumaliza muda wake wa uongozi, Yusuph Manji kuendelea kuongoza klabu hiyo.
Narudia tena kusema; ‘ Mtu mkubwa ni Mwanafunzi’, na maana alisi ya neno falsafa ni ‘ Kutafuta busara, kupenda hekima’. Falsafa linatokana na maneno mawili ya Kiyunani; ‘ Philo’ lenye maana ya ‘ Upendo juu ya jambo fulani’ na ‘ sophia’ lenye maanaya ‘ busara’.
Nyakati za kale za kirumi, mwanafalsafa alikuwa ni mtu yeyote ambaye alionesha ubingwa wa kutafakari kwa busara na hekima masuala mbalimbali.
Katika nyakati za sasa neon falsafa hutumika kuelezea mtu anayefikiri kimantiki. Falsafa ni kutafuta –busara-hekima. Kila mmoja anaweza
kufikiri kwa namna yake na kusema lolote kuhusu uamuzi wa wanacha wa klabu ya Yanga kuachana na ajenda kuu ya marekebisho ya katiba ya klabu na kutumia muda mwingi katika mkutano mkuu kumuomba mwenyekiti aliyekuwa akitakiwa kumaliza muda wake wa uongozi, Yusuph Manji kuendelea kuongoza klabu hiyo.
Ilikuwa ni kitendo cha kishujaa
kilichofanywa na wanachama hao kwa kuwa wameona kuwa wanahitaji uwepo wa
Manji ili timu yao iendelee kuwa washindani katika soka la ndani. Pia,
inawezekana wanachama hao wakawa wanahitaji kuona kiongozi huyo anabaki
ili kuhakikisha wachezaji wao nyota hawaondoki klabuni hapo.
Mambo mawili katika demokrasi,
ukiyakosa mambo hayo basi tambua hakuna demokrasia. Kwanza, kila
mwanachama alipaswa kusema kwa uhuru, na maneno ya kila mtu yanapaswa
kusikilizwa, hata kama mawazo yake hayapendwi kiasi gani. Kama mtu
anapendwa kwa wema wake, au hapendwi kwa visa vyake, hayo yote si kitu.
Kila mwanachama wa Yanga, lazima aweze kusema kwa uhuru. Watu wenye
mawazo tofauti hata wakiwa wachache, ni lazima wawe na haki ya kutoa
mawazo yao katika mkutanomkuu wa klabu bila hofu ya kusumbuliwa.
Mawazo yao yashindwe katika hoja za majadiliano. Majadiliano
yenyewe yatakayoleta uamuzi lazima yawape watu nafasi ya kusema kwa
uhuru, na hata baada ya kuamua jambo wanachama wawe na uhuru wa
kuendelea kulizungumza jambo hilo. Wal wachache wenye mawazo tofauti
lazima wafahamu kuwa kama wanayo mawazo yenye maana, na kama wakiyaeleza
mawazo hayo vizuri. Wanaweza kubadili mawazo ya wale walio wengi.
Je, wanachama wa Yanga walikuwa na haja gani na mtu ambaye walimwambia hatishiki na pesa zake mara baada ya Azam FC kufanikisha
usajili wa wachezaji, Didier Kavumbagu na Frank Domayo ,
wachezaji hao walimaliza mikataba yao na Yanga na Domayo aligoma kusaini
mkataba mpya, wakati Azam ilimuwahi Kavumbagu na kumpatia kitita kizuri
cha pesa. Walisahau yote mara baada ya Manji kutoa ufafanuzi mzuri na
kutoa ahadi kuwa ataisadia timu hiyo kufanya usajili mzuri kabla ya muda
wake wa uongozi kumalizika. Wanachama walikuwa na jabza wakati ule
lakini mbele yake wote walikuwa tayari kumuona akiendelea kuongoza klabu
hiyo.
MIMI NI mmoja wa watu
waliopendezwa na uamuzi wa pamoja wa wanachama wa klabu ya Yanga.
Ukitazama kwa umakini utagundua kuwa klabu bado inamuhitaji, Manji
ingawa yeye mwenyewe alishatamka kuwa inatosha. Inasemekana, Manji yupo
mbioni kufuata nyayo za wafadhili na viongozi mbalimbali wa klabu za
michezo ambao wamejikita katika mambo ya siasa. Ila, bado siamini kuwa
mwaka mmoja aliouomba ili kujipima kiongozi klabuni hapo atautumia
kujitangaza kiasasa kuelekea uchaguzi mkuu wa nchini, mwishoni mwa mwaka
ujao.
Ameongoza kwa miaka miwili, Yanga
na Mama, Fatma Karume alimuomba kuendelea kuwa katika nafasi hiyo kwa
miaka nane zaidi, kitu ambacho, Manji alikikataa, na hata pale
alipoombwa kuwania tena nafasi hiyo katika uchaguzi ambao kimsingi
katiba inasema unapaswa kufanyika katikati ya mwaka huu bado mwenyekiti
huyo alisema, hapana. Baada ya kuombwa sana na wanachama wa klabu, Manji
akakubali huku akitoa mapendekezo yake. Kwanza, alitaka apewe muda wa
mwaka mmoja zaidi kuendelea kuongoza.
Hapa alimaanisha uchaguzi mkuu
usogezwe mbele kwa mwaka mmoja zaidi. Kikatiba wanachama wa klabu wanayo
haki ya kusogeza mbele mkutano mkuu wa uchaguzi kama maamuzi ya pamoja
yatafikiwa na kukubaliwa. ‘ Maamuzi bab-kubwa’ yakafikiwa baada ya
wanachama kupiga kura za ‘ NDIYO’ au ‘ HAPANA’, hapo uamuzi uliofikiwa
ni kuendelea kumuongezea muda wa uongozi, Manji naye akakubali. Hiyo
ndiyo misingi ya demokrasia popote pale na Yanga wameruka ‘ kihunzi’
walichojikwaa mahasimu wao.
Pia, Manji ameomba utulivu klabuni kwa muda wote atakao kuwa madarakani, hapa alikuwa akifikisha ujumbe kwa Baraza la Wazee la
klabu kuachana na malumbano yasiyo na tija. Ni kweli, baraza
hilo linapaswa kuheshimu katiba na taratibu za klabu popote pale
wanapokuwa wakizungumza kuhusu, Yanga. Mzee, Akilimali na wenzake
wanaweza kutumia busara na hekima yao kumshahuri, mwenyekiti kwa njia za
kistaarabu, huku wakitambua mawazo yao yanaweza kukubaliwa na kufuatwa
kama yatakuwa ni mazuri, na yatawekwa kando ikiwa hayatakuwa na manufaa.
Watumie nafasi yao vizuri na si
kukimbilia katika vyombo vya habari na kuzungumza kuhusu mambo muhimu ya
klabu, tena wakiwashutumu waziwazi wachezaji pale wanapofanya makosa ya
kimchezo uwanjani. Miaka mitatu itamtosha kujua anaweza kuifanyia nini
Yanga kama atakuwa madarakani kwa miaka mine au nane ambayo ameombwa na
baadhi ya wanachama. Ndani ya uwanja Yanga ni timu iliyokaa pamoja kwa
miaka mingi hivyo itakuwa kosa kuona timu ikivurugika kwa kukosa uongozi
makini.
Mtazamo wa Manji kuhusu timu ndani ya uwanmja ni kufanya vizuri
katika michezo ya Afrika, na kwa timu iliyopo sasa na namna kiongozi
huyo anavyodili na wachezaji kama Athumani Iddi, Nadir Haroub, na
wengine ambao wakati Fulani wanasukumwa nje ya timu na wanachama wenye
jabza ni kielelezo tosha kuwa wanachama wa Yanga wamefanya maamuzi
sahihi. Sasa ni wakati wa kuyatii maamuzi hayo. Manji ana miaka miwili
tu tangu alioanza kujifunza kuhusu mambo ya uongozi wa soka, alikuwa na
sababu za msingi kuomba mwaka mmoja zaidi ili ajipime.
Kuongoza Yanga kwa siku moja ni
kazi kubwa, ila ilikuwa ni ushujaa mkubwa kwake kuona akililiwa
kuendelea kuwa mwenyekiti wa klabu hiyo. Naamini ataendelea kujifunza
zaidi na mwaka mmoja huo hautakuwa wa nia ya kujitangaza kisiasa zaidi
ya kuhakikisha Yanga inatinga hatua ya makundi ya kombe la shirikisho
barani Afrika. Uliona ukuta wa jana wa Taifa Stars? Wachezaji wanne kati
ya watano wanatoka Yanga na pengine wasingekuwepo kikosini endapo
wasingekuwa chini ya mwenyekiti mwenye upendo na busara. Yanga imevuka
salama majira haya ya usajili sasa ni kuimarisha kikosi, uamuzi
uliofikiwa uwe na utii.
0714 08 43 08
0 comments:
Post a Comment