Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
Imechapishwa Juni 2, saa 10:18 jioni
MGOMBEA aliyeenguliwa kugombea nafasi ya Urais
katika uchaguzi wa klabu ya Simba sc unaotarajia kufanyika juni 29 mwaka huu, Michael Richard Wambura, leo hii amekutana na
waandishi wa habari kujibu hoja za mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa klabu hiyo,
Mwanasheria Damas Ndumbaro juu ya kuenguliwa kwake.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini
Dar es salaam, Wambura amesema kwamba katika mkutano wa jana baina ya Ndumbaro
na vyombo vya habari alieleza mambo mbalimbali kuhusu uchaguzi wa Simba, lakini
alitumia muda mwingi kutoa hoja, shutuma na matusi mbalimbali juu yake.
Wambura amesema ni wazi maelezo yake yalilenga
kuonesha maamuzi ya kamati yake kuondosha jina lake kwenye mchakato wa uchaguzi
wa Simba sc.
Hata hivyo, Wambura alisema kwa kuzingatia katiba,
kanuni za TFF na Simba ameamua yafuatayo:
1.
“Kwakuwa nimeshakata rufaa TFF kupinga
maamuzi ya kamati ya uchaguzi ya Simba, busara inanielekeza kutokulumbana na
kujibizana na bwana Ndumbaro ili kuipisha kamati ya rufaa ya uchaguzi ya TFF
ifanye maamuzi yake.”
2.
“Kwa mambo ambayo hayana uhusiano na
uchaguzi kama kughushi nyaraka, matusi na kashfa mbalimbali mambo hayo
nitayawasilisha kwa kamati ya maadili ya TFF ili ukweli ufahamika na hatua
zichukuliwe na baada ya hapo vyombo vya dola vinavyohusiana na kutambua maandishi
vitapewa nafasi ya kufanya kazi yake.”
3.
“Ninawaomba wanachama na wapenzi wa
Simba katika kipindi hiki kuwa watulivu tukisubiri maamuzi ya kamati ya TFF na
vyombo vinavyohusika kutoa maamuzi, ni imani yangu kuwa ukweli utakuwa wazi na
haki itapatikana.”
Haya ndio majibu ya Michael Richard Wambura kwa
mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya Simba, Dkt. Ndumbaro.
0 comments:
Post a Comment