Imechapishwa Juni 10, 2014, saa 2:10 usiku
KAMISHENI ya ngumi za kulipwa Tanzania TPBC,
inataraji kufanya mkutano wa kujadili na kupitisha rasimu ya chama hicho, ili
kuhakikisha sheria na kanuni zinazopitishwa zinaeleweka kwa mabondia ambao ndio
wadau wakuu wa mchezo huo.
Mkutano huo unatarajia kufanyika Juni 22 mwaka huu
jijini Dar es Salaam
ambapo sanjari na mambo mengine utatoa mafunzo kwa mabondia juu ya
masuala mbalimbali yakiwemo sheria na kanuni za mchezo wa ngumi.
Rais wa TPBC, Chaurembo
Palasa amedai kuwa baadhi ya mabondia wamekuwa wakipigana masumbwi
pasipokuwa na ufahamu wa kutosha wa sheria za masumbwi hivyo kusababisha fujo
au kupoteza haki yao wawapo ulingoni.ambapo sanjari na mambo mengine utatoa mafunzo kwa mabondia juu ya
masuala mbalimbali yakiwemo sheria na kanuni za mchezo wa ngumi.
Chaurembo Palasa ambaye pia ni bondia wa zamani wa ngumi za kulipwa
alisema mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo mabondia katika nyanja mbalimbali za kisheria.
0 comments:
Post a Comment