Na Boniface Wambura, Dar es salaam
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa
masikitiko kifo cha aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Yanga, George Mpondela kilichotokea
jana (Juni 15 mwaka huu) katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar
es Salaam.
Kwa mujibu wa klabu ya Yanga, Marehemu Mpondela
anatarajiwa kuzikwa Alhamisi (Juni 19 mwaka huu) jijini Dar es Salaam, na msiba
upo Kigamboni Mnarani.
Mpondela alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga
katika uchaguzi uliofanyika mwaka 1994 baada ya kumshinda aliyekuwa mpinzani
wake wa karibu George Ndaombwa.
Msiba
huo ni mkubwa katika familia ya mpira wa miguu nchini kwani, Mpondela enzi za
uhai wake alitoa mchango mkubwa akiwa kiongozi katika klabu yake ya Yanga.
TFF
tunatoa pole kwa familia ya marehemu Mpondela, na klabu ya Yanga na kuwataka
kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
Taratibu
zaidi za mazishi zitatolewa na Yanga baada ya kufanya mawasiliano na familia ya
marehemu Mpondela. Bwana ametoa, Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe. Amina.
0 comments:
Post a Comment