Na Boniface Wambura, Dar es salaam
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
limepokea taarifa za kutolewa
wito bungeni wa kulitaka litumie tiketi za elektroniki katika kukusanya
mapato.
wito bungeni wa kulitaka litumie tiketi za elektroniki katika kukusanya
mapato.
Tunataka ieleweke wazi kwa umma wa Watanzania kuwa
si nia yetu
kuchelewesha matumizi ya uingiaji mpirani kwa tiketi za elektroniki. Ieleweke
kuwa mfumo wa kuingia kwenye mbuga, KCMC, mipakani ni tofauti na uingiaji
mpirani.
kuchelewesha matumizi ya uingiaji mpirani kwa tiketi za elektroniki. Ieleweke
kuwa mfumo wa kuingia kwenye mbuga, KCMC, mipakani ni tofauti na uingiaji
mpirani.
Katika mpira wa miguu wanaingia maelfu ya watu
katika kipindi kifupi. Kwa kuzingatia umuhimu wa kulinda usalama wa watazamaji
na miundombinu ya viwanja ndio maana tulisitisha matumizi ya tiketi za elektroniki
hadi tujihakikishie usalama wa matumizi yake.
Tunafanya jitihada kwa karibu na mzabuni benki ya
CRDB ili kuhakikisha mfumo huu unaanza kutumika mara moja.
Kwa niaba ya sekta ya michezo tunatoa wito kwa
Serikali kushusha au kuondoa kodi kubwa zinazotozwa kwenye vifaa vya michezo,
hasa vinavyotumiwa na watoto kuanzia umri wa miaka 6-12, ili watoto wetu waweze
kuvipata kirahisi toka kwa wazazi wao ili waweze kujifunza kucheza michezo
kisasa tangu wakiwa wadogo.
0 comments:
Post a Comment