Na Boniface Wambura, Dar es salaam
Kikosi cha Taifa Stars kinaingia tena kambini Jumatano
(Juni 11 mwaka huu) ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya raundi ya pili ya
michuano ya Afrika dhidi ya Msumbiji itakayochezwa Julai 20 mwaka huu jijini
Dar es Salaam.
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itakuwa
na kambi ya siku tatu jijini Dar es Salaam ikijumuisha wachezaji 28. Kwa mujibu
wa programu ya Kocha Mart Nooij, Stars itaingia tena kambini Juni 24 mwaka huu.
Wachezaji wanaotakiwa kuripoti kambini ni Deogratias
Munishi, Aishi Manula, Benedictor Tinoko, Kelvin Yondani, Said Moradi, Nadir
Haroub, Joram Nason, Shomari Kapombe, Oscar Joshua, Edward Charles, Aggrey
Morris na Pato Ngonyani.
Wengine ni Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Amri Kiemba,
Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Said Juma, Haruna Chanongo, Himid Mao, Said Ndemla,
John Bocco, Simon Msuva, Kelvin Friday, Ramadhan Singano, Khamis Mcha, Mrisho
Ngasa na Mwegane Yeya.
0 comments:
Post a Comment