Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
Imechapishwa Juni, 3, 2014, saa 11: 08 jioni
Timu ya
taifa ya soka Tanzania Taifa Stars, chini ya kocha Mholanzi, Mart Nooij,
inatarajia kuingia kambini Jumatano ijayo kwa ajili ya kujiwinda na mchezo
dhidi ya Msumbiji kuwania kupangwa hatua ya makundi ili kusaka tiketi ya
fainali za AFCON zitakazochezwa Morocco hapo mwakani.
Taifa Stars imewasili kutokea Harare ambako
ilifanikiwa kufuzu hatua inayofuata baada ya kuingoa Zimbabwe kwa jumla
ya magoli 3 - 2.
Stars
ilishinda bao 1-0 katika mchezo wa kwanza jijini Dar es salaam na kufanikiwa
kutoka sare ya 2-2 mjini Harare, mwishoni mwa wiki iliyopita.
Shujaa
wa Tanzania katika mchezo huo wa marudiano walikuwa ni nahodha Nadir Haroub
`Canavaro` na mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Ulimwengu.
Afisa
habari wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF, Boniface
Wambura Mgoyo amesema timu hiyo inataraji kuingia kambini kwa mara nyingine
kujiwinda dhidi ya Msumbiji Jumatano ijayo kwasababu mwalimu anatakiwa kupata
muda wa kutosha kufanyia marekebisho makosa yaliyojitokeza mechi
zilizopita.
Taifa
Stars inataraji kucheza dhidi ya Msumbiji hapo Julai 19 na 20 mwaka
huu sanjari na timu nyingine za ukanda wa CECAFA Kenya, Uganda na Rwanda ambazo
zimepenya hatua inayofuata.
Wakati huo huo, mtandao huu umekutana na John
Jambele ambaye ni miongoni mwa wadau ambao wanaonesha kufurahishwa na
matokeo bora ya Taifa Stars ambapo anawataka wachezaji hao kukaza uzi zaidi na
kutobweteka kwa hatua waliyofikia.
0 comments:
Post a Comment