Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba sc, keptein wa zamani wa JWTZ, Zacharia Hans Poppe anasubiri viongozi wapya ili awasainishe mikataba wachezaji wapya.
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
0712461976
Imechapishwa Juni 19, 2014 saa 4:08 asubuhi
KWASASA hakuna jambo la msingi kwa klabu ya Simba zaidi
ya kufanya uchaguzi wa kumpata rais mpya, makamu wa rais na wajumbe wa kamati
ya utendaji ili masuala mengine yaendelee.
Kumekuwepo na mvutano mkubwa baina ya wanachama
juu ya mizengwe inayogubika uchaguzi wa klabu hiyo, lakini chanzo cha matatizo
hayo ni pale jina la Mgombea Urais Michael Wambura lilipoenguliwa na kamati ya
uchaguzi chini ya mwenyekiti wake Wakili Dkt. Damas Daniel Ndumbaro.
Mwisho wa siku, lazima ifahamike kuwa kila palipo
na wengi pana mengi na wanapokutana watu zaidi ya wawili, lazima kutofautiana
kwa mawazo kutokee. Mivutano kama hii ni jambo la kawaida katika chaguzi za
kidemokrasia kwasababu kila mtu ana haki ya kumtetea anayemtaka.
Ukiona watu zaidi ya 100 mnakubaliana
kirahisi,kunaweza kuwa na mambo mawili, moja: kuna kiongozi wa mawazo
anayetegemewa hivyo wote mnamfuata na pili kuna uoga kwa baadhi ya watu kusema
ya moyoni.
Kuvutana ni jambo zuri kwasababu mnakosoana na
kuwekana sawa ili kufikia lengo moja. Kukosoa mtazamo wa mtu ni jambo jema wala
halina tatizo lolote. Cha msingi hoja ipingwe kwa hoja. Unayepinga hoja ya
mwenzake, alete hoja mbadala na usilete vurugu na matusi.
Hoja haipingwi kwa rungu, inapingwa kwa hoja
mbadala. Mkifanya hivyo, mbona mnafanikiwa tu.
Kwa hahati mbaya unaweza kumpenda mtu ambaye hana
haki kikatiba na kila inapotokea ndivyo sivyo kwake ukaishia kuanzisha
malumbano. Kila jambo linaendeshwa kwa misingi ya kanuni na sheria.
Kama mtu anavunja kanuni na sheria, lazima
achukuliwe hatua. Kama unampenda mvunja kanuni na sheria lazima ifike wakati uwe
mpole kwasababu makosa yanastahili hukumu.
Wachezaji
wote waliohitaji na kocha Dravko Logurusic `Loga` wameshafanya
mazungumzo na mwenyekiti wa kamati ya usajili, Hans Poppe. - See more
at: http://shaffihdauda.com/?p=2327#sthash.nkxJzXZS.dpuf
Wachezaji wote wanaohitajika na kocha Dravko Logarusic `Loga` wameshafikia makubaliana na Hans Poppe.
Lakini kama umegundua mtu wako hajatendewa haki
wakati ana haki kikatiba, basi kumpigania sio dhambi.
Suala la Wambura limekuwa tatizo katika uchaguzi
wa Simba, lakini ikumbukwe kuwa uchaguzi bora ukafanyika juni 29 kwa mazingira
yoyote yale yatayokuwepo.
Kama Wambura ana haki atagombea, kama hana haki
ataondolewa katika uchaguzi huo kwasababu kamati ya rufani inakaa leo.
Kinachowasumbua watu wengi ni kuendeshwa na
mapenzi kwa wagombea wanaowataka, hivyo kusahau kanuni na sheria za kikatiba.
Nilisema jana, Wambura alishafanya makosa siku za
nyuma kwa kuipeleka Simba mahakamani. Suala hili si la kujadili tena, FIFA
wameeleza wazi kuwa mtu anayepeleka masuala ya mpira wa miguu mahakama za
kawaida anafungiwa moja kwa moja. Lipo wazi wala halihitaji kuvunga.
Lakini tayari inaonekana uongozi wa Ismail Aden Rage
ulishafanya makosa juu ya suala hili kwa kushindwa kutekeleza maamuzi ya
kumsimamisha Wambura na kumuacha aendelee kuitumikia Simba kama mwanachama hai
huku akilipa ada.
Yote kwa yote, Simba inahitaji kupata viongozi
juni 29, binafsi naombea uchaguzi ufanyike siku hiyo ili kuinusuru klabu hiyo
na matokeo mabovu waliyoambulia misimu miwili mfululizo.
Siku za karibuni, nilizungumza na mwenyekiti wa
kamati ya usajili ya Simba, keptein wa zamani wa Jeshi la wananchi wa Tanzania,
(JWTZ), Zacharia Hans Poppe kuhusu usajili wa klabu.
Poppe alisema wanahitaji kusajili kikosi cha ushindani
ili kusaka ubingwa msimu ujao. Mwanajeshi huyo wa zamani alifafanua kuwa kamati
yake imeshaanza mazungumzo na wachezaji wanaohitajika na kocha Dravko
Logarusic.
Kwa kiasi kikubwa, Poppe alisema walishafikia
makubaliano na wachezaji wengi wanaowahitaji, kilichobaki ni kuwasainisha
mikataba, jambo ambalo ameshindwa kulifanya kwasababu anasubiri wapatikane
viongozi wapya.
Kutofanyika uchaguzi maana yake unataka Simba
isiwe bora msimu ujao kwasababu itashindwa kusajili. Poppe ana hoja ya msingi,
leo hii huwezi kuwasainisha mikataba wachezaji bila kuwa na viongozi.
Unamnunulia mtu nguo usiyejua umbo lake na rangi
aipendayo. Ikikataliwa si utakuwa umekula hasara?, bora kumsubiri rais mpya na
viongozi wapya wa chini yake. Kwahili
sina tatizo na Poppe.
Poppe mwenye mapenzi na Simba ana nia ya kuifanya Simba iwe bora
msimu ujao, lakini inategemea na viongozi watakaopatikana juni 29. Simba kuwa
na viongozi imara, hata timu itakuwa imara uwanjani. Viongozi wana uhusiano wa
moja kwa moja na wachezaji wao.
Nitaendelea kuunga mkono juhudi zinazofanyika ili
uchaguzi ufanyika juni 29, ni muhimu kuiona Simba mpya na watu wanaohusika
kuwashauri watu wanaotaka uchaguzi usifanyike, waache mara moja kwasababu hizi
ni hujuma za waziwazi,.
Sina maslahi na Simba, wala sina unazi na Simba,
lakini nina maslahi ya maandeleo ya soka la Tanzania. Kufanya vibaya kwa Simba
haiwezi kunifurahisha, lakini kufanya vizuri na kuonesha ushindani, ndio
maendeleo ya soka la Tanzania.
Simba kutikisika, ladha ya mpira wa Tanzania
inapungua. Ni timu kongwe yenye mvuto kwa mamilioni ya Watanzania.
Uchaguzi ufanyike juni 29, Zacharia Hans Poppe
afanye kazi yake kwa umakini kama alivyopanga.
Kila la kheri wekundu wa Msimbazi Simba kuelekea
uchaguzi wenu.
0 comments:
Post a Comment