Na Boniface Wambura, Dar es salaam
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa
masikitiko kifo cha mchezaji wa zamani wa timu ya Simba na Taifa Stars, Gebo
Peter kilichotokea usiku wa kuamkia leo (Juni 6 mwaka huu) katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.
Gebo aliyezaliwa mwaka 1961, pia aliwahi kuchezea timu
za Sigara ya Dar es Salaam, CDA ya Dodoma na kombaini ya Mkoa wa Dar es Salaam
(Mzizima United). Hadi mauti yanamkuta alikuwa akijishughulisha na biashara,
kubwa ikiwa ya vifaa vya michezo.
Msiba
huo ni mkubwa katika familia ya mpira wa miguu nchini kwani, Gebo enzi za uhai wake
alitoa mchango mkubwa akiwa mchezaji na baadaye kiongozi katika timu ya Manyema
ya jijini Dar es Salaam.
TFF
tunatoa pole kwa familia ya marehemu Gebo Peter, klabu ya Manyema na Chama cha
Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na kuwataka kuwa na subira na
uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
Msiba
upo nyumbani kwao Vingunguti karibu na Kanisa Katoliki ambapo taratibu za
mazishi zinaendelea kufanywa na familia.
Marehemu
ambaye ameacha mjane na watoto watatu anatarajiwa kuzikwa kesho (Juni 7 mwaka
huu) nyumbani kwao Kigurunyembe, mjini Morogoro.
Bwana
alitoa, na Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe. Amina
0 comments:
Post a Comment