Imechapishwa Juni 7, 2014, saa 3:30 asubuhi
KOCHA
Luiz Felipe Scolari amesema kitendo cha mashabiki kuwazomea wachezaji wa tiimu
ya Taifa ya Brazil katika ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Serbia jana ijumaa haina
tatizo kwake na kwa wachezaji wake kwani wapo tayari kwa mazingira kama hayo.
Selecao
walihangaika kuvunja ngome imara ya Serbia katika dimba la Sao Paulo mpaka Fred
alipofanikiwa kupenya katika dakika ya 58 na kufunga bao hilo pekee.
Mashabiki
walikosa uvumilivu na kujikuta wakiwazomea wachezaji wao kwa soka `mbofu mbofu`
dhidi ya Serbia, lakini Scolari hana tatizo na kitendo hicho.
“Ni
kitu cha kawaida,” Kocha huyo aliwaambia waandishi wa habari wa Brazil. “Ilitokea
Goiania na sehemu nyingine”.
“Haikuwa
tatizo kwa mchezaji wangu yeyote. Wako tayari kwa hili”.
“Lakini
baada ya filimbi ya mwisho, asilimia 65 ya mashabiki 67,000 waliridhishwa”.
0 comments:
Post a Comment