Kamera ziko na wewe tu: Robin van Persie akipigwa picha wakati Uholanzi wakiwasili katika hoteli yao mjini Rio de Janeiro.
Imechapishwa Juni 6, 2014, saa 1:05 usiku
BAADA ya kuwasili Rio de Janeiro jana, nahodha wa Uholanzi, Robin van Persie amejitangaza kuwa kwa asilimia 100 yuko tayari kuisaidia timu yake katika fainali za kombe la dunia mwaka huu.
BAADA ya kuwasili Rio de Janeiro jana, nahodha wa Uholanzi, Robin van Persie amejitangaza kuwa kwa asilimia 100 yuko tayari kuisaidia timu yake katika fainali za kombe la dunia mwaka huu.
Mshambuliaji
huyo wa
Manchester United alitolewa baada ya dakika 45 za kipindi cha kwanza
kumalizika katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Wales mjini Amsterdam
jumatano ya wiki hii kutokana na majeruhi, lakini amesisitiza kuwa
halikuwa tatizo kubwa na ameshachukua tahadhari nzuri.
Van
Persie aliongeza kuwa amepona kabisa majeruhi yake yake ya goti ambayo
yalimweka nje ya uwanja kwa miezi miwili wakati wa mzunguko wa pili wa
ligi kuu soka nchini England.
'Kwenye mechi dhidi ya Wales, kipindi cha pili nilikaa nje ya uwanja kwasababu mechi dhidi ya Hispania ni muhimu mno". Alisema Van Persie ambaye atawaongoza wenzake katika mchezo wa ufunguzi dhidi ya Hispania Mjini Salvador ijumaa ijayo. Inajirudia kama 2010.

Van Persie (kushoto), Nigel de Jong (katikati) na Daley Blind wakiwasili Brazil baada ya kupaa angani na ndege kwa muda mrefu.
Kocha wa Uholanzi, Louis van Gaal akifurahia mapokezi.
Kiungo wa Uholanzi, Arjen Robben akiweka saini katika T sheti ya shabiki kama ishara ya kumbukumbu.
0 comments:
Post a Comment