Wednesday, June 18, 2014


http://4.bp.blogspot.com/-CIyoW3Xt1Ww/U531sm4lXlI/AAAAAAAFq1s/q0UL2cH3jy4/s1600/2.jpg
Rais Malinzi busara zako zinahitaji kuwafanya Simba wakamilishe uchaguzi wao.

Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
0712461976

Imechapishwa Juni 18, 2014, saa 4:47

KWA misimu miwili, Wekundu wa Msimbazi wamekosa nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa barani Afrika kutokana na matokeo mabaya waliyokuwa wanayapata katika mitanange ya ligi kuu soka Tanzania bara.
Msimu wa 2012/2013, Simba waliishia nafasi ya tatu na kuipisha Azam fc katika nafasi ya pili na ubingwa kuchukuliwa na watani wake wa jadi, Dar Young Africans.
Msimu wa 2013/2014, mambo yakawa magumu zaidi na kushuhudia Simba wakiambulia nafasi ya nne na nafasi ya tatu ikichukuliwa na Mbeya City fc, huku nafasi ya pili ikitua mikononi mwa Yanga na Ubingwa ukitua Azam fc.
Kwa kushika nafasi ya tatu na nne katika misimu miwili si matokeo mazuri kwa klabu ya Simba kutokana na ukongwe wake.
Yawezekana kimpira si nafasi mbaya. Kushika nafasi ya tatu au nne katika ligi yenye timu 14 si matokeo mabaya, lakini inategemea ni timu gani imeshika nafasi hiyo.
Kwa timu nyingi za ligi kuu achilia mbali Yanga na Azam fc, kushika nafasi hizo ni mafanikio makubwa na ndio maana mara nyingi viongozi wa timu hizo utawasikia mipango yeo ni kushika nafasi ya tatu, nne na ya tano, lakini kamwe Simba na Yanga hawawezi kuwa na mipango kama hiyo.
Hadhi ya Simba na Yanga ni kuzungumziaa ubingwa tu. Kutokana na ukongwe wao, uzeofu na kusheheni mashabiki wengi, inakuwa dhambi kwa timu hizo kushika nafasi ya tatu au nne ambazo hawawezi kuwakilisha nchi katika michuano ya kimataifa.
 http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2013/11/Mwenyekiti-wa-klabu-ya-soka-ya-Simba-Ismail-Aden.jpg
Rage alipofikia na Malinzi ndio suluhisho la fukutu za uchaguzi wa Simba sc

Katika kipindi cha miaka miwili, Simba wameathirika na mambo mengi, lakini makubwa ni mabadiliko ya mara kwa mara ya benchi la ufundi na uongozi chini ya Ismail Aden Rage kushindwa kuweka umoja katika klabu.
Msimu wa 2011/2012 alikuwepo kocha Mserbia Milovan Circovic, baadaye akaja mfaransa Patric Liewig. Akiwa ameshaanza kuijenga Simba ya vijana na sasa wanaanza kumuelewa, Liewig akaondolewa na kuletwa Abdallah Kibadeni. Hawa ni walimu watatu tofauti na wana aina yao ya ufundishaji.
Wachezaji ndani ya muda mfupi walijikuta wakilishwa mifumo tofauti. Sasa walishindwa kushika kwa haraka kwasababu wakianza kuzoea kunatokea mabadiliko.
Kibadeni alikuwa ameanza kuwaweka vijana wake vizuri na tuliona Simba ikianza kutambulika na makinda wake, ghafla anatimuliwa na akaletwa Mcroatia Dravko Logarusic; Huyu naye ana mfumo wake.
Kwa mazingira haya, Simba isingeweza kutengamaa kwa haraka na walihitaji muda.
Pia uongozi wa Rage kwa muda mrefu umekuwa katika mvutano na kujikuta ukitumia muda mrefu kujibizana kwa maneno na sio kufanya kazi za klabu.
Yapo megi, lakini haya yanaweza kuwa matatizo makubwa yaliyowafanya Simba wawe hapo walipo. Lakini neema inaweza kuja kama uchaguzi mkuu wa juni 29 mwaka huu utafanyika.
Ukiwasikiliza kwa makini wanachama wa Simba, wana hamu ya kuiona klabu yao inafanya vizuri msimu ujao, na wamechukizwa na mizengwe iliyogubika uchaguzi wao.
 http://shaffihdauda.com/wp-content/uploads/2014/06/michael-wambura.jpg
Michael Richard Wambura ndio chanzo cha mvutano uliopo katika uchaguzi wa Simba na hii ilitokea baada ya jina lake kuenguliwa.

Mwishoni mwa wiki Rais wa TFF, Jamal Malinzi alisimamamisha uchaguzi wa klabu ya Simba akiitaka kamati ya utendaji iliyopo madarakani kuunda kamati ya maadili hadi ifikapo juni 30. Maamuzi hayo yalipingwa na mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi, wakili Damans Ndumbaro akidai Malinzi hana mamlaka kikatiba kusimamisha uchaguzi na kusema uchaguzi uko palepale.
Pia wanachama wengi wa Simba waliguswa na maamuzi hayo na kutoa malalamiko kwa Malinzi wakidai anaihujumu klabu yao.
Ndumabro alitaja mlolongo mrefu wa vifungu vya katiba vinavyomuondolea Malinzi nguvu ya kusimamisha uchaguzi, lakini sitavijadili kwasababu si malengo ya makala hii.
Rais wa Simba sc, Ismail Aden Rage baada ya kuona kama kuna kutunishiana misuli kati ya Ndumbaro na Malinzi, ikamlazimu kutoa ufafanuzi na kueleza kuwa ameongea na Malinzi na kumwomba uchaguzi ufanyika juni 29 kama ilivyopangwa.
Rage aliongea kwa busara na kumuangukia Malinzi kwasababu kubwa moja ambayo ni kwamba; dirisha la usajili limefunguliwa tangu juni 15 mwaka huu, lakini Simba wamesimama kusajili mpaka wapate viongozi wapya.
Kutofanyika uchaguzi juni 29 ni kuithiri Simba kwa kiasi kikubwa. Wanatakiwa kupatikana viongozi haraka iwezekanavyo ili usajili uendelee.
Ukisikiliza pande zote mbili, kila upande unaongea yake, lakini mwisho wa siku, mgombea wa Urais aliyeenguliwa, Michael Richard Wambura ndio chanzo cha yote haya.
Kuenguliwa kwa jina lake ndio kumeleta mizengwe katika uchaguzi wa Simba, lakini sio muda muafaka wa kuanza kulizungumzia hili. Ni wazi Wambura aliwahi kufanya makosa katika klabu hiyo ambapo kubwa zaidi ni kuipeleka Simba mahakamani.
Sheria za FIFA ziko wazi, mambo ya mpira hayatakiwa kupelekwa mahakama za kawaida. Kisheria Wambura alijiondoa kwenye masuala ya mpira alipofanya hivyo.
Lakini kuna makosa yaliendelea kufanyika kwa Wambura kuachwa na viongozi wa Simba akifanya shughuli za klabu ikiwemo kulipa ada. Kitendo hiki kilimpa nguvu ya kurudishwa kwenye uchaguzi na kamati ya rufani ya TFF ya Wakili Julius Lugaziya baada ya kuenguliwa. Kumbuka mpaka sasa ni mjumbe wa kamati ya utendaji iliyopo madarakani.
Cha msingi kwa Rais Malinzi ni kutambua kuwa Simba inategemea sana busara za TFF ili kufanikisha uchaguzi wake. Kwa walipofika na mazingira halisi ya sasa, hakuna jinsi ya kuzuia uchaguzi huo.
Ni jambo la faraja kusikia Rage na Malinzi wamekubaliana uchaguzi ufanyike, na mimi nilitegemea hivyo kwasababu ndio njia ya kuinusuru Simba kwa sasa.
Simba ni klabu kubwa, inapokuwa mbovu, ladha ya ligi kuu inapungua kama ilivyo kwa wenzao Yanga. Kuna faida ya kuwa na Yanga na Simba imara katika ligi.
Misimu miwili mashabiki wa Simba wameumia vya kutosha, ipo haja ya kuwaacha wafanye uchaguzi ili wasajili vizuri kwa lengo la kurejesha makali yao.
Huu si muda muafaka wa kuendelea kuandika mvutano wa Wambura na kamati ya Ndumbaro, Rage na wanachama wa Simba, Kamati ya uchaguzi na TFF,ni muda muafaka wa kutoa mawazo ya kuwasaidia Simba wafanye uchaguzi juni 29.
Rais Malinzi wewe ni baba wa mpira wa Tanzania. Hakuna mtu wa juu zaidi yako TFF. Kwa lugha nyepesi wewe ndio mtu wa mwisho kama ilivyo kwa rais wa nchi.
Maneno yako yana nguvu sana, jambo la msingi kwako ambalo ni ushauri wa bure ni kwamba; kila unapofanya maamuzi kumbuka wewe ni baba, lazima uangalie athari itakayotokea.
Si jambo zuri hata kidogo kuona watu wanakupinga hadharani ukiwa Rais. Tamko lako linatakiwa kuwa na nguvu, inapotokea unapingwa, basi kikazi linakushushia heshima.
Sina wasiwasi na utendaji wako, lakini kuna mambo yanafanyika na watu kuanza kukuwazia vibaya. Kwa mfano kwasasa kuna maneno mengi yakikuhusisha kumbeba Michael Wambura. Yawezekana sio sahihi, lakini matendo yanayotokea ndio yanafikisha jambo hili hapa lilipo.
Cha msingi, wape Baraka zote simba, tena bila kinyongo ili wafanye uchaguzi, bila kufanya hivyo, klabu hii inaweza kuingia kwenye mgogoro mkubwa.
Simba inagusa maisha ya watu wengi. Ndio maana ni rahisi watu kuzimia inapofanya vibaya uwanjani,. Hii ni klabu iliyojaa mioyoni mwa watu. Waacheni wafanye uchaguzi.
Hizo sheria mnazotumia kubishana kufanya maamuzi ifike wakati sasa uchaguzi ufanyike. Kama mtu hana vigezo aondolewe, lakini kama ameonewa basi apatiwe msaada wa kisheria.
Nawatakia kila la heri Simba katika uchaguzi wa juni 29. Ni matumaini yangu baada ya hapo mtasajili kikosi kizuri.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video