Imechapishwa Juni 3, 2014, saa 2: 14 asubuhi
KOCHA
mkuu wa Nigeria, Stephen Keshi ametaja kikosi chake cha mwisho cha wachezaji 23
kwa ajili ya kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.
Mabingwa
hao wa soka barani Afrika wanaenda kushiriki fainaili hizo kwa mara ya tano na
wamepangwa kundi moja na Argentina, Iran na Bosnia.
Wachezaji
wazoefu kama Vincent Enyeama, Austin Ejide, Joseph Yobo na Elderson Echiejile waliokuwa sehemu ya kikosi cha fainali za
mwaka 2010 nchini Afrika kusini wamejumuishwa katika orodha hiyo ya mwisho.
Mfungaji
bora wa fainali za 29 za AFCON, Emmanuel Emenike, Godfrey Oboabona, John Obi
Mikel na Victor Moses wanatarajia kucheza fainali zao za kwanza za kombe la
dunia.
Kikosi
kizima:
Walinda
mlango:
Vincent Enyeama, Austin Ejide, Chigozie Agbim
Walinzi: Joseph Yobo, Elderson Echiejile, Juwon Oshaniwa, Godfrey Oboabona, Azubuike Egwuekwe, Kenneth Omeruo, Efe Ambrose, Kunle Odunlami
Walinzi: Joseph Yobo, Elderson Echiejile, Juwon Oshaniwa, Godfrey Oboabona, Azubuike Egwuekwe, Kenneth Omeruo, Efe Ambrose, Kunle Odunlami
Viungo: John Mikel Obi,
Ogenyi Onazi, Ramon Azeez, Michael Uchebo, Reuben Gabriel
Washambuliaji: Osaze Odemwingie,
Ahmed Musa, Shola Ameobi, Emmanuel Emenike, Babatunde Michael, Victor Moses,
Uche Nwofor
0 comments:
Post a Comment