Imechapishwa Juni 1, 2014, saa 12:01 jioni
BAADA ya kuachwa na Vicente del Bosque, Jesus Navas na Daniel Carvajal wamewatakia kila la heri
wachezaji wenzao wa timu ya taifa ya Hispania kueleka kutetea ubingwa wao wa
kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.
Navas aliachwa katika kikosi chake na kocha
alieleza kuwa sababu ni kutokuwa fiti baada ya kupona majeruhi ya kifundo cha
mguu siku za karibuni.
Nyota huyo mwenye miaka 28 akucheza mchezo wa mwisho
wa ligi kuu nchini England mwezi aprili, lakini amesema amafurahi sana
kwasababu ameimarika.
“Ninajivunia kuimarika kwangu kwa wakati muafaka
na nilitegemea kulitetea taifa langu nchini Brazil”. Ameandika Navas katika
mtandao wake wa Twita.
“Nawatakia kila la kheri wachezaji wenzangu na
kocha wangu mafanikio makubwa katika kutetea ubingwa”.
Naye beki wa Real Madris, Carvajal alikuwa
miongoni mwa wachezaji wa kikosi cha awali cha wachezaji 30 kabla ya kuachwa
katika kikosi cha mwisho.
Beki huyo ametwiti: “ Ni aibu kukosekana katika
kikosi cha mwisho, lakini najivunia kwasababu nilikuwa karibu kutajwa. Nawatakia
Hispania kila la heri”.
Wakati huo
huo kiungo wa Atletico Madrid, Koke amefurahi kujumuishwa katika kikosi cha
Hispania baada ya kufanya vizuri katika michuano ya UEFA na kwenda kushiriki
fainali zake za kwanza za kombe la dunia.
“Nimefurahi kuchaguliwa kwenda Brazil, nitakuwa
makini kuisaidia timu yangu”.
0 comments:
Post a Comment