Mwimbaji wa Brazil, Maria Rita (kushoto, mbele), mwanamitindo Fernanda Lima (kulia, mbele ) wakitumbuiza katika mkutano huo.
SAO
PAULO, Brazil
Rais wa
shirikisho la soka duniani, FIFA, Sepp
Blatter amefungua mkutano wa 64 wa shirikisho hilo, mjini Sao Paulo jana jioni.
Maofisa
wa juu wa FIFA, mashirikisho sita wanachama wa FIFA na wanachama 206 vya vyama
walihudhuria mkutano huo.
Blatter
pamoja na Wazili wa michezo wa Brazil, Aldo Rebelo walitoa hotuba zao kwenye
mkutano huo wakizungumzia fainali zinazoanza kesho nchini Brazil.
Mkutano
huo uliambatana na zawadi mbalimbali, burudani kutoka kwa wasanii na mambo
yaliiva zaidi pale mshambuliaji wa zamani wa Ufaransa mwenye miaka 80 kwa sasa,
Just Fontaine alipozawadiwa kiatu cha Adidas chenye madini ya almasi.
Nyota
huyo alifunga mabao 13 katika mechi sita za kombe la dunia lililofanyika nchini
Sweden mwaka 1958 na kuiongoiza Ufaransa kushika nafasi ya tatu, huku akiibuka
mfungaji bora wa pekee katika historia ya fainali za kombe la dunia. Rekodi
yake haijavunjwa mpaka leo.
Picha hii ilipigwa jana juni 10, 2014 wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 64 wa FIFA.
Kwa
kuwa fainali za 1958 hazikuwa na zawadi ya kiatu cha dhahabu, Fontaine alisema
jana usiku kuwa kiatu hicho ni zawadi maalum kwa mke wake na timu yake ya
Ufaransa.
Muda
wa jioni, wawakilishi mbalimbali, Josephine King (OFC), Hassan Shehata (CAF),
Mirabror Usmanov (AFC), Jozef Venglos (UEFA), Maria Coto (CONCACAF), Carlos
Valderrama (CONMEBOL) na Antonio Mattarese (FIFA) walipata
nafasi kuzungumza machache.
Kabla
ya kufungua mkutano huo, kamati ya utendaji ya FIFA ilikaa kikao mjini Sao
Paulo na kuwahakikishia Brazil kuwa watapa msaada kamili kutoka shirikisho hilo
na wana imani nao kwa uwezo mkubwa walioonesha kuandaa kombe la dunia
linaloanza kutimua vumbi kesho mjini Sao Paulo.
Pia Kamati
ya utendaji katika mkutano huo iliwasilisha kanuni 10 za mpira wa miguu wa
wanawake ikihitaji zipitishwe.
Mshambuliaji wa zamani wa Brazil, Edson Arantes do Nacimento "Pele" akijibu maswali mjini Sao Paulo
Kuhusu
kashfa za rushwa wakati wa upigaji kura
ya kumpata mwenyeji wa fainali za kombe la dunia kwa mwaka 2022, kamati ya
utendaji ilisema suala hilo liachwe katika kamati ya maadili ili imalize kazi
yake kabla ya kutoa msimamo wake.
Pia
mkutano huo ulibariki maamuzi ya kuzisaidia Bosnia na Herzegovina, Croatia,
Romania na Serbia msaada wa dola za kimarekani milioni mbili ili kuimarisha
miundombinu ya soka ambayo iliharibiwa na mafuriko makubwa siku za karibuni.
Pia
kamati ilithibitisha kuwa Mexico itaibadili Canada katika fainali za Olympik za
soka la vijana la wanawake zinazotarajia kufanyika China mwaka huu.
Mkutano
huo wa FIFA unamalizika leo jioni.
0 comments:
Post a Comment