Kampuni ya Bin Slum Tyre Company Limited leo imeingia mkataba
rasmi wa kuidhamini timu ya soka ya Mbeya City Council ya jijini Mbeya
katika hafla fupi ya utiaji saini mkataba huo iliyofanyika katika ukumbi
wa ofisi za jiji la Mbeya, Mkataba huu utakuwa wa miaka miwili, ambao
utawafanya Mbeya City kunufaika na kiasi hicho cha fedha kwa muda huo
wote wa mkataba.
Mkataba
huo wenye thamani ya milioni 360 ambao kampuni hiyo itakuwa ikitangaza
bidhaa za RB Battery katika jezi za timu ya Mbeya city, na pia chini ya
namba nyuma ya jezi itaandikwa kampuni ya Bin Slum Tyre Company.
Akiongea
wakati wa utiaji saini wa mkataba huo jijini Mbeya, Mkurugenzi wa ,
Binslum Tyre Mohamed Binslum, alisema “Tumefikia makubaliano haya baada
ya kuona uongozi wa timu ya Mbeya City umejipanga vizuri katika
kuendesha timu yao, na kupata mwitikio mkubwa kutoka kwa wananchi wa
Jiji la Mbeya pamoja na mikoa ya Kanda ya Kusini, hivyo itakuwa ni fursa
nzuri kwa kuzitangaza betri zetu za RB ambazo pia Mbeya ni soko letu
kubwa”.” Kampuni yetu ina bidhaa nyingi kama vile aina nzuri ya matairi
ya Double Star na Vee Rubber”. Aliongeza Binslum.Meya wa jiji la Mbeya Mheshimiwa Athanas Kapunga, ameishukuru kampuni ya Binslum kwa kukubali kuingia mkataba huo ambao utaisaidia timu kuongeza ufanisi wa kuindesha timu yao. “Napenda kuishukuru mkurugenzi wa Binslum Tyre Company Limited kupitia betri za RB kwa kuonyesha nia ya dhati katika kuedeleza soka la jiji la Mbeya na Tanzaniam kwa ujumla, nina imani msimu ujao tutakuwa na uwezo na kasi kubwa sana kama vile taa za gari zinavyotoa mwanga wa taa mkali zikiwa na betri za RB”. Alisema Meya wa jiji la Mbeya.
Naye Meneja masoko na uhusioano wa jamii wa kampuni ya Binslum Tyre Bw. Peter Ngassa alisema “Binslum Tyre Company tumeamua kuwekeza katika mpira wa miguu Tanzania kwa sababu kuna nafasi nzuri ya kutangaza bidhaa zetu kupitia eneo hilo na kutoa matokeo chanya pia kwa Mbeya City kutimiza ndoto zao”. Pia kupitia betri imara za RB tunaitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete anaoutoa kila mara akiagiza makampuni mbalimbali kujitokeza kudhamini michezo kwa njia mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment