
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
Imechapishwa Juni 10, 2014, saa 1:40 usiku
MUDA wowote kutoka sasa bomu la Michael Richard
Wambura linaweza kulipuka baada ya taarifa za ndani kueleza kuwa mvutano
umekuwa mkali baina ya wajumbe wa kamati ya rufani ya shirikisho la soka
Tanzania, TFF juu ya kurudi au kuondolewa kwa mgombea huyo katika nafasi ya
urais kwenye uchaguzi wa Simba unaotarajia kufanyika juni 29 mwaka huu.
Wambura alikata rufani kupinga maamuzi ya kamati
ya uchaguzi ya Simba chini ya mwenyekiti wake, Wakili, Damas Ndumbaro akipinga
kuenguliwa kwenye mchakato wa uchaguzi.
Mgombea huyo aliondolewa kwasababu kubwa mbili,
moja ni kuipeleka Simba mahakamani na pili ni kusimamishwa uanachama wake.
Mtandao huu upo maeneo ya tukio kufuatilia `ngado
kwa ngado` na mara taarifa rasmi itakapotoka, itatolewa kwa wadau wote.
Kumekuwepo na taarifa nyingi zinasambazwa na watu
mbalimbali kuwa Wambura anarudi na wengine wanasema anaondolewa, lakini ukweli
ni kwamba taarifa rasmi kutoka ndani ya Hotel ya Courtyard, Upanga, jijini Dar
es es salaam, haijatoka.
Zoezi lilioanza mchana wa leo ni kuyapitia maelezo
ya pande zote na mpaka muda huu bado maamuzi hayajawekwa hadharani na wajumbe
bado wapo ndani ya ukumbi.
Ngoma ya Wambura inaonekana nzito, lakini mwisho
wa siku lazima maamuzi yafikiwe.
Endelea kuwa nasi na tutawapeni taarifa rasmi muda
wowote zitakapotoka, ingawa kuna taarifa za chini ya kapeti kuwa Wambura
anarudi.
Taarifa hizi si rasmi, hivyo zinaweza kuwa sahihi
au zisiwe sahihi kwasababu bado kuna usiri mkubwa kutoka ndani ya ukumbi.
0 comments:
Post a Comment