Atakubali?:
Michael Richard Wambura rufani yake imekataliwa na kamati ya Rufani ya uchaguzi
ya TFF baada ya kubainika alipiga kampeni kabla ya muda ikiwa ni mara ya pili
anafanya kosa hilo. Mara ya kwanza yeye na Evans Aveva walipewa onyo kali
la maandishi baada ya kumwaga sera siku ya kuchukua na kurudisha fomu.
Atakubali?:
Michael Richard Wambura rufani yake imekataliwa na kamati ya Rufani ya
uchaguzi ya TFF baada ya kubainika alipiga kampeni kabla ya muda ikiwa
ni mara ya pili anafanya kosa hilo. Mara ya kwanza yeye na Evans Aveva
walipewa onyo kali la maandishi baada ya kumwaga sera siku ya kuchukua
na kurudisha fomu. - See more at:
http://shaffihdauda.com/?p=2389#sthash.tiR7NQFB.dpuf
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
0712461976
Imechapishwa Juni 20, 2014, saa 4:50 asubuhi
KAMATI ya Rufani ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeikataa rufani ya Michael Wambura kupinga kuenguliwa kugombea urais katika uchaguzi wa klabu ya Simba unaotarajiwa kufanyika baadaye mwezi huu.
KAMATI ya Rufani ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeikataa rufani ya Michael Wambura kupinga kuenguliwa kugombea urais katika uchaguzi wa klabu ya Simba unaotarajiwa kufanyika baadaye mwezi huu.
Wambura aliwasilisha rufani yake mbele ya Kamati hiyo
iliyokutana jana (Juni 19 mwaka huu) jijini Dar es Salaam chini ya Kaimu
Mwenyekiti Wakili Mwita Waissaka kupinga uamuzi wa kumwengua katika
kinyang’anyiro hicho uliofanywa na Kamati ya Uchaguzi ya Simba kwa kufanya
kampeni kabla ya muda uliopangwa.
Baada ya kupitia vielelezo, kanuni na sheria, Kamati
ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF imeridhika kuwa mrufani (Michael Wambura) alifanya
kampeni kabla ya muda kinyume na Ibara ya 6(1)(a) na (g), Ibara ya 6(1)(l)
pamoja na Ibara ya 14(3) ya Kanuni za Uchaguzi za TFF toleo la 2013.
Kwa mujibu wa ibara hizo, Kamati ya Uchaguzi ya Simba
inayo mamlaka ya kumwengua (disqualify) mgombea anayefanya kampeni ama kukiuka
maagizo halali ya Kamati ya Uchaguzi.
Uamuzi wa Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF
umezingatia Katiba ya TFF pamoja na kanuni zake, na pia Katiba ya Simba.
Kwa namna moja ama nyingine suala hili limegusa hisia
za baadhi ya wanachama wa Simba hususani wenye mapenzi na Michael Wambura.
Rais
wa TFF, Jamal Emil Malinzi (kushoto) alisema jana suala la uchaguzi wa Simba
litapatiwa ufumbuzi na akapongeza juhudi za Aden Rage kuwasiliana kwa ukaribu
na shirikisho, kauli iliyoonekana kuwawashia Simba taa ya kijani.
Baadhi ya wanachama wa Simba walikuwa wanampigania
Wambura ili agombee urais na hii ilidhihirika wakati ule alipoenguliwa na
kamati ya uchaguzi ya Simba sc. Mengi yalizungumzwa, lakini mgombea huyu
alikata rufani na kushinda na hatimaye kurudishwa katika mchakato wa uchaguzi.
Kabla ya kupeleka Rufani yake TFF, Wambura alikutana
na waandishi wa habari na kueleza kutoridhishwa na maamuzi ya kamati ya
uchaguzi chini ya mwenyekiti wake, Wakili Dkt. Damas Daniel Ndumbaro na kusema
anakata rufaa kupinga.
Kweli alikata rufaa na kurejeshwa kwenye uchaguzi. Kwa
wanaomuunga mkono Wambura ilikuwa furaha kwao kuona anaendelea kuwania Urais.
Kwa wanaompinga pengine ilikuwa pigo kwao.
Pande zote mbili zilitambiana hususani wa upande wa
Wambura. Kwa bahati mbaya sana, mgombea baada ya kurudishwa na kamati ya rufani
ya uchaguzi ya TFF alikutana na waandishi wa habari na kuelezea furaha yake ya
ushindi.
Lakini sijui ni kujisahau au ni kuzidi kwa furaha,
wakati namsikiliza Wambura siku ile, alitamka maneno ambayo binafsi nilihisi
yatahusishwa na kampeni. Ni maneno ambayo hayakustahili siku ile, nilijua
Wambura ataeleza tu furaha yake ya kushinda, na kusema anasubiri muda wa
kampeni ufike.
Kabla ya hapo, Wambura na Aveva walishapewa onyo kali
baada ya kupiga kampeni siku ya kuchukua na kurudisha fomu. Aveva amekuwa
mjanja kwani toka siku hiyo hajasikika tena, zaidi ya watu wanaosemekana
kumuunga mkono, wakitajwa `Friends of Simba`.
Nilitegemea Wambura kuwa mtulivu baada ya kushinda
Rufani, sijui marafiki zake walimshauri nini. Lakini kilichoonekana ni kutaka
kupambana na Azim Dewji ambaye kabla alimponda Wambura na kusema hafai kuwa
Rais wa Simba kwasababu hataki wafadhili.
Kamati
ya Rufani ya TFF inayoongozwa na mwenyekiti wake, Wakili Julius Mutabazi
Luzaziya (kushoto) imeamua kukataa rufani ya Michael Wambura, japokuwa wakili
Lugaziya hakuwepo jana.
Azim sio mgombea na kwa bahati Mbaya katiba ya Simba
ina mapungufu kwa hili, haina namna ya kumbana mwanachama anayepiga kampeni
kabla ya muda, Hata katibu wa kamati ya uchaguzi ya Simba, Khalid Kamguna
alikiri mapungufu haya na kusema watawashauri viongozi wajao wafanyia
marekebisho katiba na kuingiza kipengele cha kumbana mwanachama kama Azim mara
atakapoongea maneno kama yake wakati kampeni bado.
Wambura alistahili kupima upepo kwasababu kamati ya
uchaguzi ya Simba ina mtu mfuatiliaji kama Ndumbaro. Namjua wakili huyu
kwasababu amenifundisha somo la `media Law` chuo kikuu cha Dar es salaam. Ni
mtu mwenye msimamo na anatumia sana sheria kuamua mambo yake. Nilijua suala la
Wambura atalichukulia kwa uzito na kumfuatilia nyendo zake kama mwenyekiti wa
kamati.
Baada ya Wambura kushinda rufani, Ndumbaro hakusema
chochote, lakini aliendelea kumfuatilia na kama alijua udhaifu wa Wambura ni
katika kuzungumza mambo bila kuzingatia wakati. Simsemi vibaya, lakini
alihitaji kuwa mtulivu ili kukwepa mitego ya kamati ya uchaguzi ya Simba.
Kwa bahati mbaya, Wambura akajikoroga wakati anamjibu
Azim. Kosa hilo limesababisha kiama chake hapo jana baada ya kuondoshwa kwa
kosa la kupiga kampeni kabla ya muda, na safari hii sio kuipeleka Simba
mahakami na kusimamishwa uanachama.
Kigingi hicho alikwepa, lakini akajisahau na
kujichinja mwenyewe. Sidhani kama kamati ya Rufani imeogopa, naamini kanuni
zimetumika na binafsi nilitegemea matokeo ya hivyo.
Haya yameshatokea, jambo la msingi ni Simba kufanya
uchaguzi wao. Kwa siku mbili zilizopita nimeandika kuwa hakuna jinsi ya kuzuia
uchaguzi wa Simba kutokana na mazingira halisi.
Simba inatakiwa kupata viongozi ili isajili wachezaji
kwa ajili ya ligi kuu msimu ujao. Kuchelewesha uchaguzi ni kuiumiza klabu. Hata
maamuzi ya Rais, Jamal Malinzi kusimamisha uchaguzi sikuyaunga mkono hata kama
alikuwa na mamlaka.
Nilisema Kwamba, Malinzi alihitaji busara kuisaidia
Simba kufanya uchaguzi, na kwa bahati nzuri yeye ni muungwana, jana alionesha
dhahiri ameshakubali uchaguzi ufanyike na ndio maana aliruhusu kamati ya Rufani
ya uchaguzi isikilize rufaa ya Wambura.
Jambo la msingi ni wanachama kupiga kura juni 29.
Wambura kama atabahatika kusoma makala hii, ushauri wa bure ni kukubali
kilichotokea kama kweli ana mapenzi na Simba na anataka kuiona inafanikiwa
msimu ujao.
Akiamua kupambana tena kwa kuona ameonewa, mwisho wa
siku, klabu yake anayoipenda itaharibikiwa. Nina amini bado ana mawazo na
mchango mkubwa kwa klabu. Haitakuwa dhambi kuendelea kutoa mchango wake hata
akiwa nje ya uongozi.
Sidhani kama kiongozi pekee ndiye anaweza kuisaidia
klabu. Japokuwa ni kweli kuwa lazima awepo mtu wa kuwaongoza wenzake, lakini
naamini Wambura asukumwe na busara ili aache uchaguzi ufanyike na maisha
mengine yaendelee.
Michael Richard Wambura, yawezekana hajapenda na
kukubaliana na maamuzi ya kamati ya Rufani ya uchaguzi ya TFF, lakini kumbuka
hao hao ndio walikupa ushindi kwasababu waliona una haki.
Hao hao wamekuondoa kwa mara ya pili baada ya kugundua
una makosa. Ni busara kukaa pembeni kuliko kuendeleza sinema hii ambayo unaweza
kulaumiwa na wanasimba wengi mara mambo yatakapokuwa mabaya.
Wanachama wanaompenda Wambura, kumbukeni kuna kushinda
na kushindwa. Mlishinda mara ya kwanza, wenzenu wakaumia. Sasa wao wameshinda,
waacheni waendelee na uchaguzi na ninyi nendeni
mkachague. Hakuna haja ya kususia uchaguzi eti kwasababu mnayempenda
kaondolewa.
Simba ni yenu wala sio ya Wambura wala Aveva wala
Tupa. Mkigombana kwasababu ya wagombea, haitawasaidia kuijenga klabu. Mgombea
mmoja ameondoshwa, angalieni waliobaki, mtakayemuona anafaa mchagueni kwa
manufaa ya klabu yenu.
Kila la kheri Simba sc katika uchaguzi wenu.
0 comments:
Post a Comment