Imechapishwa Juni 12, 2014, saa 4:03 asubuhi
MAZOEZI ya Argentina jana jumatano yalivamiwa na mtu moja mwenye sura inayofahamika duniani.
MAZOEZI ya Argentina jana jumatano yalivamiwa na mtu moja mwenye sura inayofahamika duniani.
Wakati Lionel
Messi na wachezaji wenzake wakijiandaa kuelekea mchezo wa ufunguzi wa kundi lao dhidi ya Bosnia siku ya jumapili, shabiki mmoja mwenye sura inayofanana na nyota wa zamani wa Brazil, Ronaldinho alivamia uwanjani.
Waargentina walimfurahia jamaa huyo lakini alitolewa na maofisa wa uwanja.




Mashabiki wengi walivamia uwanjani na kumpigia magoti nahodha huyo wa Argentina, Lionel Messi huku wakifuta viatu vyake.
Messi alicheka tu na aliwakumbatia mashabiki hao na alimpa shabiki mmoja sweta lake kabla ya walinzi kumtoa.


Ajabu! mamia ya mashabiki wa Argentina walifurika uwanjani wakati timu yao ikijiandaa na mchezo wa ufunguzi wa kundi F dhidi ya Bosnia.
0 comments:
Post a Comment