Hoi : Kiungo wa Ujerumani, Marco Reus akiwa ameshika kifundo chake cha mguu wa kushoto baada ya kuumia katika mchezo dhidi ya Armenia
Reus akitibiwa na madaktariwa timu ya taifa ya Ujerumani.
Reus akitolewa uwanjani kwa matibabu zaidi.
Imechapishwa Juni 7, 2014, saa 3:10 asubuhi.
PIGO!, Marco Reus hatihati kucheza fainali za kombe la dunia baada ya jana kupata majeruhi ya kifundo cha mguu katika ushindi wa mabao 6-1 ambao Ujerumani ilivuna dhidi ya Armenia ikiwa ni pasha pasha kabla ya kuanza kombe la dunia wiki ijayo.
PIGO!, Marco Reus hatihati kucheza fainali za kombe la dunia baada ya jana kupata majeruhi ya kifundo cha mguu katika ushindi wa mabao 6-1 ambao Ujerumani ilivuna dhidi ya Armenia ikiwa ni pasha pasha kabla ya kuanza kombe la dunia wiki ijayo.
Nyota
huyo Borussia Dortmund alianguka chini baada ya kugongana na kiungo wa
Armenia, Artur Yedigaryan na kuambulia kuumia na kuzua hofu kubwa kwa
mashabiki wa Ujerumani na benchi zima la ufundi.
Reus
aliachwa amelala chini kwa maumivu makali na kupatiwa matibabu uwanjani
kabla ya kutolewa katika mchezo huo kabla ya muda wa mapumziko.
Nyota huyo mwenye miaka 25 aliripotiwa kushindwa hata kuvaa kiatu katika mguu wake wa kushoto na imeelezwa kuwa alipelekwa moja kwa moja hospitali kwa ajili ya uchunguzi wa kina.
Joachim Low anajiandaa kucheza na Ureno juni 16 katika mechi ya ufunguzi, na inawezekana Reus akazikosa fainali za kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.
Akizungumza baada ya mechi, Low alisema: "Tuna matarajio kuwa atapona. Lakini inaonekana kuwa mbaya sana. Tunaweza kumuita mchezaji mwingine saa 24 kabla ya mchezo wa kwanza".
Hofu: Bosi wa Ujerumani, Joachim Low (wa tatu kutoka kushoto) alionekana kuwa na wasiwasi baada ya Reus kutolewa nje ya uwanja.
Reus alipigwa picha kabla ya kupata majeruhi jana dhidi ya Armenia.
0 comments:
Post a Comment