Mwenyekiti wa Yanga SC - Yusuf Manji akiongea na wanachama wa kwenye Ukumbi wa Bwalo la Poilisi - Oysterbay
Imechapishwa Juni 1, 2014, 2: 48 usiku
Mkutano Mkuu wa marekebisho ya baadhi ya vipengele kwenye Katiba ya Yanga umefanyika na kumalizika salama na furaha kwenye Ukumbi wa Bwalo la Polisi -Oysterbay huku wanachama wakipitisha kipengele cha kuundwa kwa kamati ya maadili.
Mwenyekiti wa klabu ya Yanga SC Yusuf Manji amewaongoza wanachama hai
wapatao 1,560 kupitisha kipengele hicho kipya kwa ajili ya maslahi na
faida ya Wana Yanga kwani bila kufanya hivyo timu isingeweza kuruhusiwa
kushiriki Ligi Kuu msimu ujao.
Aidha
katika mkutano huo Manji amewatoa hofu wanachama kwa kuwaambia kuwa
usajili unaendelea kufanyika na nafasi zilizobakia ni nne tu hivyo pindi
utakapokamilika basi wataweka wazi kila kitu.
Kuhusu
nafasi ya Kocha Mkuu Manji amesema Kamati ya Mashindano imemkabidhi
mapendekezo yao na kwa sasa yupo kwenye mazungumzo na Marcio Maximo
aliyewahi kuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa Tanzania kuja kukinoa kikosi
cha Jangwani.
Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini Mama Fatma Karume
aliongoza kikao cha waachama kilichomuomba Bw Manji kuendelea na uongozi
ambapo mwenyeikti alitoka nje na kamati yake ya utendaji na pindi
waliporejea walikubali ombi hilo na kusema watafuata taratibu za
kikatiba.
Mwisho kupitia mkutano mkuu wa leo wa wanachama
umeazimia kuwaongezea muda wa mwaka mmoja Mwenyekiti Yusuf Manji pamoja
na Makamu wake Clement Sanga ili waweze kukamilisha masuala ya katiba na
kuweza kuandaa mkutano wa uchaguzi baada ya katiba kupitishwa na TFF.
0 comments:
Post a Comment