Shabiki makini: Mchumba wa Mario Balotelli, Fanny Neguesha alikuwa miongoni mwa mashabiki wa Italia dhidi ya England.
Imechapishwa Juni 15, 2014, saa 11: 31 asubuhi
MSHAMBULIAJI mtukutu, Super Mario Balotelli macho yake hayakuwa kwa taifa lake tu, bali hata kwa mchumba wake Fanny Neguesha ambaye alikuwa miongoni mwa mashabiki waliofurika katika mchezo wa ufunguzi wa Italia wa kundi D dhidi ya Simba watatu, timu ya taifa ya Engaland.

Katika
mechi hiyo ambayo Balotelli aliifungia Italia bao katika ushindi wa
2-1, mchuchu wa nyota huyo alivalia jezi namba 9 ya Italia yenye jina la
basha wake, Balotelli.
Neguesha
kwa muda wote alikuwa na tabasamu baada ya mpenzi wake kufunga bao safi
kwa kichwa mapema kipindi cha pili na kuifanya Italia iwe mbele kwa
mabao 2-1.
Mambo safi!: Neguesha akifurahia hali ya hewa mjini Manaus na kupiga picha kwa simu yake.
Tabasamu tupu: Neguesha akipunga mkono kwenye screen kubwa ya uwanjani wakati Italia ikiiadabisha England.
Mmiliki wa `totoz zuri`: Balotelli (katikati) alianza katika kikosi cha Italia kwenye mechi ya ufunguzi dhidi ya England mjini Manaus
Rasmi: Balotelli alitangaza kumchumbia Neguesha kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram jumatatu ya wiki hii.
0 comments:
Post a Comment