Thursday, June 12, 2014



http://4.bp.blogspot.com/-yGL1bYozPoE/U5h4qU2zHCI/AAAAAAACz34/Mab3sYp1_4w/s1600/Pix-1.JPG
Mwenyekiti wa kamati ya Rufani ya TFF, Wakili Julius Mutabazi Lugaziya (kushoto) alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jana kutangaza kutengua maamuzi ya kamati ya uchaguzi ya Simba kuliengua jina la Wambura.

Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
0712461976

Imechapishwa Juni 12, 2014, saa 11:14 jioni

BAADA ya kamati ya rufani kutengua maamuzi ya kamati ya uchaguzi wa Simba sc kuhusu kuliengua jina la Mgombea Urais, Michael Richard Wambura na kumrudisha katika kinyang`anyiro hicho mengi yanazungumzwa juu ya uhalali wa maamuzi hayo.
Ulikuwa mlolongo mrefu mpaka kufikia maamuzi. Kamati ya rufani ilikaa kwa siku mbili, lakini ngoma ilikuwa nzito mpaka walipoamua kupiga kura ambapo Wambura alipata kura 3 kati ya 5 za wajumbe wa kamati.
Baadhi ya watu wanaeleza kuwa kamati ya Rufani ya TFF imembeba Wambura na wengine wanahoji kwanini maamuzi hayo yamefikiwa kwa njia ya kura wakati kanuni na sheria zipo wazi.
Mwenyekiti wa kamati ya Rufani, Wakili Julius Mutabazi Lugaziya alifafanua jana kuwa kwa kawaida maamuzi ya vikao vya rufani, inapofikia wajumbe wanashindwa kufikia muafa, maamuzi yanaamuriwa kwa kura.
Jana wakati Wakili Lugaziya akiongea na waandishi wa habari kutangaza maamuzi ya kamati yake, alizungumza mambo mengi ambayo baadhi yake niliyaandika kwa kirefu.
 https://fbexternal-a.akamaihd.net/safe_image.php?d=AQBo4mAbL0WPkZ6o&w=484&h=253&url=http%3A%2F%2Fptblog.pesatimes.com%2Fwp-content%2Fuploads%2F2014%2F05%2Fnnnn.jpg&cfs=1&sx=0&sy=26&sw=640&sh=335
Michael Richard Wambura anaungwa mkono na wanachama wengi wa Simba sc

Ikumbukwe sheria za mpira wa miguu ziko wazi kabisa. Ni dhambi kubwa kupeleka masuala ya mpira wa miguu katika mahakama za kawaida. Jambo hili lilifanywa na Wambura miaka ya nyuma. Kwa sheria ilivyo, mtu anayefanya haya anajiondoa katika masuala ya mpira wa miguu.
Moja ya mapingamizi aliyowekewa Wambura, suala la kuipeleka Simba Sports Club mahakamani katika kesi Namba 100/2010 iliyofunguliwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es salaam, Kinyume na Ibara ya 11 (1) (e), (2), 12(3), na 55 ya Katiba ya Simba Sports Club ya Mwaka 2010 lilikuwa na nguvu na wengi waliokuwa wanaamini ataondolewa moja kwa moja katika uchaguzi wa Simba waliegemea sehemu hii.
Pia kamati ya uchaguzi ya Simba sc, chini ya mwanasheria, Dkt. Damas Ndumbaro, ilieleza kuwa sababu nyingine ya kumuengua Wambura ni kwamba, mwekewa Pingamizi (Wambura) alisimamishwa Uanachama na Kamati ya Utendaji ya Simba Sports Club iliyokutana tarehe 5 Mei 2010 na barua ya tarehe 6 Mei 2010, (Kumb. Na. SSC/MMKT/163/VOL.40/11) na hivyo basi anapoteza haki za kuwa mwanachama wa Simba Sports Club.
Sababu hizi mbili ndio zilikuwa na nguvu katika maamuzi ya kamati ya uchaguzi ya Simba sc kuliengua jina la Wambura.
Baada ya maamuzi hayo, Wambura alikata rufani kupinga maamuzi akiweka sababu 14 na hapo jana ndipo majibu ya rufani yake yalitoka na kushinda.
Wambura aliipekea Simba mahakamani, hilo halina ubishi. Wambura alisimamishwa uanachama, hilo pia linafahamika. Lakini je, baada ya kusimamishwa, utekelezaji wa adhabu hiyo ulikuwaje?, hapo ndipo tatizo lilipoanzia.
 http://freemedia.co.tz/daima/wp-content/uploads/2014/05/wambura_61.jpg
Katiba ya Simba iko wazi na inaeleza kuwa mtu ambaye amepoteza uanachama, hatakiwa kushiriki shughuli yoyote ya klabu. Haya yameandikwa kwenye katiba ambayo wanasimba wanayo na wanaisoma kila siku.
Walimsimamisha uanachama, lakini wakamuacha aendelee kushiriki kazi za Simba ikiwemo mikutano mikuu na ya dharuta, pamoja  na vikao vya maamuzi ya klabu ya Simba.
Kamati ya rufani ilieleza kuwa Wambura tangu asimamishwe, amekuwa akishiriki shughuli za Simba kama mwanachama halali.
Wakili Lugaziya alisema katika mikutano minne iliyofanyika nyuma Wambura alishiriki akiwa mwanachama halali na kubwa zaidi mpaka leo ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya klabu ya Simba.
Wambura alishiriki katika mkutano wa mabadiliko ya katiba, pia alihusika kuiteua kamati ya uchaguzi ambayo baadaye ilimuengua.
Lugaziya alifafanua kuwa kinachoonekana hapa ni kwamba, baada ya Simba kumsimamisha Wambura, haikuwahi kumchukulia kama amesimamishwa kwasababu amekuwa akishiriki shughuli za Simba.
“Katiba inasema mtu anayepoteza uanachama, anapoteza haki ya kulipa ada, kushiriki mikutano na vikao vya maamuzi na kupoteza haki ya kuteuliwa katika vyombo mbalimbali vya Simba sc”.
“Wambura tangu atangazwe kusimamishwa amekuwa akilipa ada na michango yote ya uanachama na michango ya mawazo kwa kipindi chote, isipokuwa kunapokuwa na uchaguzi”. Alisema Wakili Lugaziya.
Aliendelea kwa kusema kuwa  pili; Wambura ameshiriki mikutano yote mikuu na ya dharura kwa kipindi chote. Ikumbukwe kuwa ni sharti la msingi la katiba kuwa mwanachama halali yaani ambaye ni hai kwa maana ya yule aliyelipa ada yake na hajasimamishwa ndiyo anatakiwa kushiriki tu.
“Uongozi wa klabu ya Simba ulikuwa na mamlaka ya kuhoji mahudhurio ya mwanachama asiye halali, hilo halijawahi kufanyika kwa Wambura”.
“Tatu; Mrufani amewahi kuteuliwa na kushiriki  kuandaa mpango mkakati wa Simba sc ulioshirikisha chuo kikuu huria. Kamati hiyo ilishirikisha wajumbe ambao sio wanachama wa Simba sc, hata hivyo kamati haikushawishika kuwa mrufani aliitwa kama mtu `baki`, bali aliona kuwa bwana Wambura aliitwa kwa kuzingatia nafasi yake ndani ya samba sc.”
“Kubwa zaidi Mrufani mpaka hivi sasa ni mjumbe wa kamati ya utendaji. Ameshiriki kufanya maamuzi mengi ikiwemo kuchagua kamati ya uchaguzi yenyewe pamoja na mkutano wa katiba. Mwanachama asiye na haki anawezaje kufanya mambo haya yote na wenzake wanaangalia?”. Alihoji Wakili Lugaziya.
“Suala la uanachama wa mrufani (Wambura) halijawahi kuhojiwa ama kwa mujibu wa mrufani mwenyewe au mwanachama mwingine yeyote wa Simba sc. Jambo alilosimamishia mrufani lilikuwa la dharura. Kwa mujibu wa katiba ibara ya 12, suala hilo lilitakiwa kuletwa katika mkutano mkuu unaofuata”.
 http://ptblog.pesatimes.com/wp-content/uploads/2014/05/52.jpg
Siku Wambura alipochukua fomu ya kugombea Urais Simba sc

“Mrufani alisimamishwa tarehe 5 mei mwaka 2010, mkutano mkuu wa Simba sc uliofuata ulifanyika siku nne baadaye, yaani tarehe 9, 5, 2010. Hoja ya kusimamishwa ikiwa bado inatokota wakati ule mkutano ulipofanyika, hata hivyo hoja hiyo haikuwasilishwa kwenye mkutano ule na mikutano mingine mingi iliyofuata. Kwa kushindwa kufanya hivyo, kamati ya utendaji na si mrufani, ilishindwa kutekeleza matakwa ya katiba na mbaya zaidi badala ya kuchukua hatua zilioainishwa ikawa inampa fursa mbalimbali kutoa michango yake Simba sc”.
“Kwa mujibu wa katiba ya Simba, kamati ya utendaji inakutana mara moja kila baada ya miezi mitatu, kwa maana hiyo kwa mujibu wa katiba ya Simba ibara ya 31 kifungu cha kwanza, kamati ya utendaji inakutana mara nne kwa mwaka”.
“Tangu mei 2010 ukitoa miezi mitatu iliyokuwa imepita, kamati ya utendaji ya Simba inatakiwa kuwa imekaa vikao vya kikatiba 20. Kwa mujibu wa katiba hiyo ibara ya 20, mkutano mkuu unafanyika mara moja kwa kila mwaka, tangu wakati huo imefanyika mikutano mikuu ya kawaida minne, mrufani (Wambura) ameshiriki mikutano yote hiyo”.
“Kwahiyo kamati ya rufani imejielekeza kwenye kanuni zinazozuia mtu au chombo kukanusha mambo iliyoyafanya kwa maana ya kwamba kwa kutangaza kuondoa haki za mwanachama, lakini hapo hapo ikawa inampa haki na kushiriki kama mwanachama, ni kama vile yenyewe iliondoa zuizi lake na haina nafasi ya kumkanusha mwomba rufani”
“Kamati ilijielekeza katika athari ya kuutunza uamuzi wa kamati ya uchaguzi wa Simba. Endapo chombo au kikao chochote kimefanya maamuzi na baadhi ya wajumbe walioshiriki katika chombo kile hawakupaswa kushiriki katika uamuzi, uamuzi uliopitishwa unakosa nguvu za kisheria. Kama ndivyo kamati ikajiuliza, je, vikao vilivyoandaa katiba ya Simba na kuipitisha ambayo mrufani (Wambura)alishiriki vina athari zipi kuhusu uhalali wa katiba yenyewe ya Simba.
“Pili; Je, vikao vilivyoteua kamati ya uchaguzi ya Simba ambavyo mrufani alishiriki huku akiwa hana hadhi ya kushiriki vina maanisha nini katika uhalali wa kamati wenyewe.”
“Kama mtu batili ameshiriki kupitisha maamuzi, yale maamuzi nayo yanakuwa batili. Kwa maana hiyo kama tutaendelea kutunza uamuzi wa kamati ya uchaguzi ambayo na yenyewe ni batili.  kwa maana hii, katiba ya Simba haipo kihalali, Je, athari hizo zingeleta matokeo gani?”.
“Lakini kamati ilishasema huko nyuma kuwa Simba leo hii haiwezi kukataa kwamba ilimchukuliwa Wambura kama mwanachama wa kawaida wa Simba. Kwahiyo suala la ubatilifu linakuwa halipo”.
“Kamati inapenda ieleweke kwamba uamuzi huu hauna maana na wala usichukuliwe kwa maana yoyote ile kwamba una nia ya kufungua njia kwa wanachama wa klabu kupeleka masuala ya mpira kwenye mahakama hizi za kawaida”.
“Maana ya maamuzi haya ni kwamba,  uamuzi huu unalenga kuzihimiza klabu mwanachama wa TFF kuzingatia taratibu walijiwekea kwa uweledi badala ya kutumia taratibu hizo kwa manufaa hasi na kwa manufaa ya wachache kwenye mpira wa miguu”.
“Kwasababu tulizozitaja na tutakazofafanua zaidi kwenye waraka tutakaoutoa, kamati ya rufani ya uchaguzi ya TFF inabatilisha uamuzi wa kamati ya uchaguzi ya Simba sc. Michael Richard Wambura anastahili kuwa mgombea na kuondolewa kwake kunatenguliwa”.
Haya ndiyo yalikuwa maelezo ya mwenyekiti wa kamati ya rufani ya TFF, Wakili Julius Mutabazi Lugaziya hapo jana.
 http://4.bp.blogspot.com/-ETDvqlntEHM/UZ-JVjUICaI/AAAAAAAAiKE/WXB-09kKauQ/s1600/Pix-4.jpg
Ismail Aden Rage (kulia), uongozi wake ulishindwa kusimamia taratibu za katiba kuhusu suala la Michael Wambura

Ukiyafuatilia kwa umakini maelezo na sababu walizotumia kumrudisha Wambura, unagundua kuwa kuna usahihi na hoja ndani yake.
Wambura alikuwa na makosa, lakini kuna upande mmoja ulishindwa kufanya kazi yake kwa maana ya uongozi wa klabu ya Simba.
Miaka ya nyuma, baadhi ya wanachama walipiga kelele kwe mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage juu ya uhalali wa Wambura na wengine walikuja juu zaidi alipoteuliwa kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji.
Baadhi yao walihitaji ufafanuzi juu ya uteuzi ule, lakini wakati anateuliwa, tayari alikuwa ameifanyia Simba mambo mengi kwa nafasi ya uanachama.
Nadhani hata wale waliokuwa wanafuatilia suala hilo ilifika wakati wakalipotezea kwasababu ni utamaduni wa watanzania wengi kuwaka kwa muda na kuachana na jambo muhimu.
Mambo mengi yanatokea katika jamii ya watanzania, watu wanaongea, lakini inafika muda wanaacha na kuendelea na maisha mengine. Hivi ndivyo suala la Wambura lilivyoshughulikiwa katika klabu ya Simba.
Wambura ni mtu maarufu, anafahamika na watu wengi, hivyo akienda kwenye mkutano ni rahisi kutambulika. Angekuwa mtu wa kawaida, labda tungesema hakuonekana, lakini bado kulikuwa na daftari la mahudhurio.
Wanachama wa Simba walikuwa wanamuona Wambura kwenye mikutano yao na akifanya kazi muhimu za klabu, lakini hawakuwahi kuhoji kwa umakini na kuhakikisha wanapata majibu.
Kwa bahati mbaya baada ya uongozi wa Rage kushindwa kuwajibu kwa wakati, inawezekana wakaona sio `ishu`. Lakini madhara yake yamekuwa makubwa.
Kama kweli kamati ya Lugaziya ingetunza maamuzi ya kamati ya uchaguzi ya Simba, hakika mambo yangekuwa mengine. Maana yake uhalali wa katiba ungehojiwa na kamati ya uchaguzi yenyewe.
Fikiria kama wangebatilisha kila kitu, nini kingetokea kwa wakati huu. Ingeleta athari kubwa mno. Binafsi naomba uamuzi wa kamati ya rufani uheshimike.
Yanazungumzwa mengi kwasababu ni haki ya mtu kueleza mawazo yake, lakini tuwe wepesi wa kukubali makosa na kuanza upya.
Simba tayari walishafanya makosa siku za nyuma, Wambura amekuwa mjanja zaidi yao.. Lazima wanachama wakubaliane na hilo.
Hakuna jinsi kwa sababu zilizoelezwa, cha msingi muacheni Wambura aende kwenye uchaguzi kupambana na Evans Aveva na Andrew Tupa.
Kama akishindwa basi, kama atashinda isiwe kigezo cha kugombana. Kura ndio mwamuzi wa yote. Wingi wa kura utampa urais Wambura au uchache wa kura utamnyima Urais.
Wanachama wa Simba, tulieni na achaneni na maneno yasiyokuwa na msingi kwa muda huu, nendeni mkafanye maamuzi juni 29 mwaka huu.
Nawatakia amani wanasimba wote wakati huu muhimu wa uchaguzi.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video