Oscar Tabarez amesema watu wasitarajie kumuona Luis Suarez akianza katika kikosi chake dhidi ya England.
Imechapishwa Juni 19, 2014, saa 1:01 usiku
KOCHA wa Uruguay , Oscar Tabarez
amesema Luis
Suarez anaendelea kuimarika baada ya kufanyiwa upasuaji, lakini amekiri
kuwa mshambuliaji huyo hataweza kucheza kwa kiwango kama alichoonesha
akiwa ligi kuu.
Mshambuliaji
huyo wa Liverpool amekuwa akisumbuliwa na majeruhi ya goti, lakini
baada ya kufungwa na Costa Rica anatarajia kucheza dhidi ya England
maarufa kama Simba watatu.
Tabarez amegoma kuweka wazi kama ataanza katika mechi hiyo na amewataka mashabiki kuwa wavumilivu juu ya nyota wao.
Anaimarika: Mshambuliaji huyu anaweza kuanza katika mechi muhimu ya kundi D dhidi ya England
Anaimarika: Mshambuliaji huyu hatari anaweza kuwavaa England licha ya kuwa na matatizo ya goti.
Presha? Kikosi cha Oscar Tabarez kilichapwa mabao 3-1 dhidi ya Costa Rica katika mchezo wa ufunguzi wa kombe la dunia nchini Brazil
Diego Lugano alitolewa katika mchezo, lakini Tabarez anasema mbinu zake hazitabalika.
Tabarez pia aligoma kutaja kikosi chake kwa ajili ya mechi ya kundi D itakayocheza leo ambapo mchezaji Diego Lugano ndiye atakosekana.
"Kama atacheza (Suarez) lazima tukubali kuwa hatakuwa fiti kama alivyokuwa ligi kuu," alisema Tabarez. "Hata kama hatakuwa fiti kwa asilimia 100, ni mtu anayeweza kutoa mchango mkubwa kwa timu".
"Tunadhani kama kila kitu kitakwenda vizuri, hakuna sababu ya yeye kutocheza kombe la dunia. Ameimarika vizuri".
0 comments:
Post a Comment